Naseeb Abdul Juma Issack, maarufu kama Diamond Platnumz, ni msanii mahiri wa Bongo Flava, mnenguaji, mfanyabiashara, na mfadhili ambaye ameendelea kudhihirisha uwezo wake—sio tu katika muziki, bali pia katika ulingo wa biashara.
RELATED: Diamond Platnumz – Nitafanyaje (Prod. S2kizzy)
Baada ya kusubiriwa kwa muda mrefu na kuacha mashabiki wakiwa na maswali kibao kuhusu “mzigo” alioupokea, hatimaye amezindua rasmi bidhaa yake mpya ya sabuni inayoitwa “Wasafi Soap.” Kupitia ukurasa rasmi wa Instagram wa Wasafi Soap, ametangaza ujio wa sabuni hii bora inayozingatia mahitaji ya kila Mtanzania, ikilenga usafi na ulinzi wa mazingira.
Sasa, Wasafi Soap inapatikana katika maduka yote nchini, ikikupatia fursa ya kuchagua sabuni yenye ubora wa hali ya juu, inayotunza afya na kuzingatia hali halisi ya maisha ya Mtanzania. Kama unahitaji usafi wa kipekee, basi Wasafi Soap ni chaguo lako—“Usafi kama wote!”
Also, check more tracks from Diamond Platnumz;