LIFESTYLE

Tazama Matokeo ya Kitado Cha Nne 2024/2025 hapa

Tazama Matokeo ya Kitado Cha Nne 2024/2025 hapa

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza rasmi matokeo ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika Novemba 2024. Kwa mujibu wa Katibu Mtendaji wa NECTA, Dkt. Said Mohamed, jumla ya watahiniwa wa shule 477,262 kati ya 516,695 waliofanya mtihani wamefaulu, ikiwa ni sawa na asilimia 92.37 ya watahiniwa wote wenye matokeo.

RELATED: Jay Melody – Wa Pekee Yangu

Dkt. Mohamed alitangaza matokeo hayo leo, Januari 23, 2025, jijini Dar es Salaam. Alieleza kuwa kiwango cha ufaulu kimeongezeka kwa asilimia 3.01 ikilinganishwa na mwaka 2023, ambapo watahiniwa 471,427 walifaulu, sawa na asilimia 89.36.

Kati ya watahiniwa waliofaulu mwaka huu:

  • Wasichana: 249,078, sawa na asilimia 91.72 ya wasichana wote wenye matokeo.
  • Wavulana: 228,184, sawa na asilimia 93.08 ya wavulana wote wenye matokeo.

Link inayofunguka ya Matokeo ya Kidato cha nne 2024

LINK 1: Tazama matokeo ya kidato cha nne hapa

LINK 2: Tazama matokeo ya kidato cha nne hapa

Dkt. Mohamed aliipongeza jamii ya elimu nchini, ikiwemo walimu, wanafunzi, na wadau wote, kwa kufanikisha ongezeko hili la ufaulu. Pia alisisitiza umuhimu wa kuendelea kuboresha mazingira ya elimu na kuweka juhudi zaidi ili kuhakikisha viwango vya ufaulu vinaendelea kupanda katika miaka ijayo.

Also, check more tracks from Jay’s melody;

Leave a Comment