LYRICS

Harmonize – Nitaubeba Lyrics

Harmonize - Nitaubeba Lyrics
Harmonize – Nitaubeba Lyrics

VERSE 1
Imagine uko jangwani umepotea mchana juani unatembea
Utokapo ni mbali uendapo ni mbali
Mara ngamia mbebaji akatokea na kukushusha mzigo uliokuelemea
Upate afadhali pole na safari

And that’s why today to me yote tisa ila kumi umeonesha maana ya upendo
Si kwa maneno bali kwa vitendo
Umeridhika na nilichonacho vya watu hutoleagi macho
Siku nikiwa sina twalala Oooh baby twalala

Aaaah baby if I close my eyes mi namuomba Mungu akulinde
Na akusimamie we ndo pacha wangu mie

BRIDGE
Eti siku hizi vipi mbona sikusikii tena, sikusikii ukilia sikusikii ukisema
Niko busy na boo jamani nimeshasema, niko busy na baby na msalaba wake

CHORUS
Nitaubeba, nitaubeba nitaubeba na ntafika nao kiume
Nitaubeba (iwe kwenye shida na raha) nitaubeba (ama kwenye shibe na njaa)
La kwako ndo langu my darling na ntafika nao kiume

VERSE 2
Imagine hujifahamu umezimia umewekewa damu zinaingia
Bomba ikafunguka na huwezi hata nyanyuka
Mara dakitari wa zamu akaingia umepata fahamu unamwangalia
Machozi yanakuanguka unatamani funguka

And that’s why today to me yote tisa ila kumi unanifurahisha kwenye tendo
Au unipe penzi la magendo

Aaaah baby if I close my eyes mi namuomba Mungu akulinde
Na akusimamie we ndo pacha wangu mie

BRIDGE
Eti siku hizi vipi mbona sikusikii tena, sikusikii ukilia sikusikii ukisema
Niko busy na boo jamani nimeshasema, niko busy na baby na msalaba wake

CHORUS
Nitaubeba, nitaubeba nitaubeba na ntafika nao kiume
Nitaubeba (iwe kwenye shida na raha) nitaubeba (ama kwenye shibe na njaa)
La kwako ndo langu my darling na ntafika nao kiume

OUTRO
Iwe kwenye shida na raha ama kwenye shibe na njaa
La kwako ndo langu my darling

1 Comment

  • Umeitsha sana kwenye Lyrics.

    Ila naomba hapa uichange mbadala wa kua

    “And thats why today to me yote tisa ila kumi umeonesha maana ya upendo“

    Iwe

    And thats what you did to me yote tisa ila kumi umeonesha maana ya upendo.

    Keep up the good work.

Leave a Comment