SPORTS

Matokeo Kamili Ya Yanga Vs Pamba Jiji Leo 03 Oktoba 2024

Matokeo Ya Yanga Leo Dhidi Ya Pamba Jiji 03 October 2024

Mabingwa watetezi, Yanga SC, wameendelea kuonyesha ubabe wao baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Pamba Jiji FC kutoka Mwanza, katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara uliofanyika usiku huu kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, jijini Dar es Salaam.

RELATED: Kikosi cha Yanga Leo Dhidi Pamba Jiji 03 October 2024

Mabao ya Yanga yalifungwa na:

  • Ibrahim Hamad Abdallah ‘Bacca’ dakika ya 5,
  • Stephane Aziz Ki, aliyefunga kwa penati dakika ya 45′ + 2,
  • Maxi Mpia Nzengeli dakika ya 54,
  • Kennedy Musonda dakika ya 85.

Kwa ushindi huo, Yanga wanafikisha jumla ya pointi 12 baada ya michezo minne, huku Pamba Jiji ikisalia na pointi zake nne baada ya kucheza michezo saba. Yanga SC wameshinda mechi zao zote na wanaendelea na rekodi yao ya kutopoteza mechi 20 mfululizo, huku wakiweka karatasi safi (clean sheets) katika michezo 7 iliyopita. Ushindi huu ni ishara ya utawala wao wa soka katika ligi ya msimu huu wa 2024/2025.

Matokeo Kamili Ya Yanga Vs Pamba Jiji Leo 03 Oktoba 2024

Pamba Jiji, ambao walikuwa wakitafuta matokeo bora, walikumbana na changamoto nyingine baada ya beki wao Saleh Abdullah kutolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 44 kufuatia kadi ya pili ya njano kwa kumchezea rafu beki wa Yanga, Mkongo Chadrack Isaka Boca. Kutokana na kucheza pungufu, Pamba Jiji walishindwa kuhimili kasi na shambulizi la Yanga, na safu yao ya ulinzi ilipata wakati mgumu kuzuia mashambulizi ya mabingwa hao watetezi.

RELATED: Kikosi cha Pamba Jiji dhidi ya Yanga Leo – 03 Oktoba 2024

Yanga wameonyesha kuwa bado ni timu ya kutisha kwenye Ligi Kuu ya NBC, huku wakiendeleza utawala wao dhidi ya wapinzani wao wa ndani.

Citimuzik inaendelea kukuletea matokeo ya moja kwa moja, takwimu za mechi, na maoni ya kina. Endelea kufuatilia mechi zote za Ligi Kuu NBC kwa habari za wakati halisi na utiririshaji wa moja kwa moja unapopatikana.

Matokeo Kamili Ya Yanga Vs Pamba Jiji Leo 03 Oktoba 2024

Je, Yanga SC wataendelea kutamba msimu huu? Tafadhali, endelea kuwa nasi kwa habari zaidi!

Leave a Comment