SPORTS

Kikosa Kipya Cha TAIFA STARS Dhidi Ya Congo – AFCON

Kikosa Kipya Cha TAIFA STARS Dhidi Ya Congo - AFCON

Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, inajiandaa kuingia kambini kwa ajili ya michezo miwili muhimu ya kufuzu michuano ya AFCON 2025 dhidi ya DR Congo. Mechi ya kwanza itachezwa Oktoba 10, 2024, ambapo Stars itaanzia ugenini, na mechi ya pili itapigwa nyumbani Tanzania, tarehe Oktoba 15, 2024.

RELATED: Msimamo wa Ligi Kuu Bara 2024/2025 – NBC Premier League Tanzania

Katika maandalizi haya, mshambuliaji mahiri wa klabu ya PAOK ya Ugiriki, Mbwana Samatta, amejumuishwa kwenye kikosi cha Taifa Stars. Hii inakuja baada ya yeye na Simon Msuva kukosekana katika kikosi kilichocheza dhidi ya Ethiopia na Guinea mnamo Septemba 4 na 10, 2024.

DR Congo inaongoza kundi H kwa alama 6, ikifuatiwa na Tanzania yenye alama 4, Ethiopia ikiwa na alama 1, na Guinea ikiwa haina alama.

Kikosa Kipya Cha TAIFA STARS Dhidi Ya Congo – AFCON
  • Ally Salim (Simba SC)
  • Zuberi Foba (Azam FC)
  • Yona Amos (Pamba SC)
  • Mohamed Hussein (Simba SC)
  • Lusajo Mwaikenda (Azam FC)
  • Pascal Msindo (Azam FC)
  • Ibrahim Hamad (Young Africans)
  • Bakari Nondo (Young Africans)
  • Dickson Job (Young Africans)
  • Abdulrazak Hamza (Simba SC)
  • Haji Mnoga (Salford City, Uingereza)
  • Adolf Mtasingwa (Azam FC)
  • Habib Khalid (Singida Black Stars)
  • Himid Mao (Talaal El Geish, Misri)
  • Mudathiri Yahya (Young Africans)
  • Feisal Salim (Azam FC)
  • Suleiman Mwalim (Fountain Gate FC)
  • Cyprian Kachwele (Vancouver Whitecaps, Canada)
  • Clement Mzize (Young Africans)
  • Mbwana Samatta (PAOK FC, Ugiriki)
  • Kibu Dennis (Simba SC)
  • Nasoro Saadun (Azam FC)
  • Abdullah Said (KMC FC)

Kocha Mkuu: Hemed Suleiman

RELATED: Harmonize – Yanga Bingwa

Tunategemea mchezo mkali na wa kuvutia kutoka kwa Taifa Stars wakati wanapoendelea na kampeni ya kufuzu AFCON 2025. Endelea kufuatilia TFF TV na TFF Radio kwa habari na matangazo ya moja kwa moja.

Play fair, and Be Positive!

Also, check more tracks from Harmonize;

Leave a Comment