SPORTS

Matokeo ya Yanga 1 vs 0 KMC Leo 29 Septemba 2024 – Ligi Kuu

Matokeo ya Yanga 1 vs 0 KMC Leo 29 Septemba 2024 - Ligi Kuu

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania, Yanga SC, leo wanawakaribisha KMC FC kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi. Mchezo huu wa Ligi Kuu unatajwa kuwa ni “Jumapili ya Kufosi”, huku mashabiki wa Yanga wakitarajia kuona timu yao ikiendeleza rekodi nzuri ya ushindi.

RELATED: Harmonize – Sherehe (Prod. S2kizzy)

Yanga inakutana na KMC huku wakiwa na kumbukumbu bora ya ushindi mnono wa msimu uliopita, ambapo kwenye mechi mbili walizokutana, Yanga walishinda kwa jumla ya mabao 8. Agosti 23, 2023, Yanga walitoka na ushindi wa 5-0 wakiwa wenyeji, huku Februari 17, 2024, waliporejea tena dimbani, wakiibuka na ushindi wa 3-0, safari hii wakiwa ugenini.

Matokeo ya Yanga 1 vs 0 KMC Leo 29 Septemba 2024 – Ligi Kuu

Dakika ya 5 ya mchezo, Max Nzegeli aliifungia Yanga goli la kwanza na pekee la mechi. KMC walijitahidi kurudi mchezoni, lakini safu ya ulinzi ya Yanga ilionekana imara na haikuruhusu nafasi nyingi za mabao. Kipindi cha pili kilianza bila mabadiliko makubwa, na Yanga walifanikiwa kumaliza mechi kwa ushindi wa 1-0.

Rekodi za Yanga Dhidi ya KMC

Katika michezo 12 ya Ligi Kuu waliyokutana, Yanga wameibuka washindi mara 9, huku KMC wakipata ushindi mara moja tu, na mechi mbili zikiishia kwa sare. Rekodi hizi zinathibitisha ubabe wa Yanga dhidi ya KMC na zinaweza kuipa Yanga motisha zaidi ya kuendelea kutawala kwenye mchezo wa leo.

Msimu wa 2024/2025 kwa Yanga

Yanga imeanza msimu huu kwa moto, ikishinda mechi zao mbili za kwanza bila kuruhusu bao lolote kufungwa, huku wakifunga mabao 3. Timu hiyo imekuwa na ukuta imara, wakiruhusu bao moja tu katika mechi nane za mashindano mbalimbali tangu msimu uanze, huku safu yao ya ushambuliaji ikifunga mabao 25 katika mechi hizo. Kiwango hiki kimeifanya Yanga kuwa tishio kwa timu pinzani.

Mazingira ya Mechi

Yanga wanaingia kwenye mechi hii wakiwa na morali ya juu baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar ugenini na ushindi wa 1-0 dhidi ya KenGold katika mchezo uliopita wa ligi. Kwa upande wa KMC, hali yao si nzuri msimu huu, wakiwa wameshinda mechi moja tu, sare moja, na kupoteza mechi tatu. Wamefunga mabao matatu na kuruhusu saba, jambo linaloashiria udhaifu katika safu yao ya ulinzi.

Hata hivyo, mchezaji wa kutegemewa wa KMC, Redemptus Musa, ameibuka kuwa nyota wa timu hiyo msimu huu kwa kufunga mabao mawili kati ya matatu ya timu yake. Anaonekana kuwa tegemeo la KMC katika mchezo huu, huku akiwa na jukumu kubwa la kuvunja safu ya ulinzi ya Yanga.

Historia ya Mechi za Yanga Dhidi ya KMC
  • Mechi: 12
  • Yanga Imeshinda: 9
  • KMC Imeshinda: 1
  • Sare: 2
  • Magoli Yanga Wamefunga: 21
  • Magoli Yanga Wamefungwa: 5
  • Clean Sheets za Yanga: 7
Umuhimu wa Mchezo

Kwa Yanga, ushindi huu utawasaidia kuendelea kuongoza kwenye msimamo wa Ligi Kuu na kuimarisha nafasi yao ya kutetea ubingwa. Kwa KMC, ni nafasi ya kurekebisha mwenendo wao mbaya wa msimu huu na kupata alama muhimu, ingawa wanakutana na changamoto kubwa dhidi ya mabingwa watetezi.

Leave a Comment