C - NEWS

TANZIA: Marco wa Zabron Singers Afariki Dunia

Marco wa Zabron Singers Afariki Dunia
Marco wa Zabron Singers Afariki Dunia

Kulingana na taarifa, Mwimbaji wa kundi la Zabron Singers, Marco Joseph Bukuru amefariki dunia. Marco alikuwa mwanachama wa kikundi cha Zabron Singers, ambacho ni maarufu kwa nyimbo za Injili, hususan wimbo wao maarufu “Sweetie Sweetie”. Alikuwa na mchango mkubwa katika muziki wa Kikristo nchini Tanzania.

RELATED: Wanawake Jasiri Walioleta Mapinduzi Katika Hip Hop Tanzania

Shemeji wa marehemu, Tecla Lucas, ameiambia Mwananchi leo, Agosti 22, 2024, kwamba mwili wa marehemu bado upo kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali hiyo, wakisubiri kupanga ratiba za mazishi.

Tecla amesema, “Marehemu amefariki kutokana na ugonjwa wa moyo akiwa Hospitali ya Muhimbili jana usiku. Msiba utafanyika Mikocheni kwa mama yake mdogo, na kwa sasa mwili bado upo kwenye chumba cha kuhifadhia maiti.”

Leave a Comment