ENTERTAINMENT

Senga Achafukwa, Amjibu Mzee Magoma wa Yanga πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Senga Achafukwa, Amjibu Mzee Magoma wa Yanga πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

MCHEKESHAJI mkongwe, Ulimboka Mwalulesa, almaarufu kama Mzee Senga, ameshindwa kujizua na kufunguka maneno makali dhidi ya Mzee Magoma wa Yanga na sakata zima la kesi. Hii ni baada ya Mzee Magoma na wenzake kushinda kesi dhidi ya Yanga na kudaiwa kuvunja uongozi uliopo, wakitaka wakabidhiwe timu hiyo ya Yanga.

RELATED: Diamond Platnumz – Mtasubiri Ft Zuchu (Prod. Lizer)

Hata hivyo, Yanga walijibu kwa madai kuwa Mzee Magoma na wenzake walifoji sahihi za viongozi wengine, hivyo kupelekea kushinda kesi hiyo. Pia, Yanga wameomba kuongezewa muda ili kuchunguza zaidi juu ya kesi hiyo. Hali hii imezua hasira kwa mashabiki wengi wa Yanga na kusababisha pia Mzee Senga kucharuka.

Sakataa hili limeleta taharuki kubwa ndani ya klabu ya Yanga, huku mashabiki wakisubiri kwa hamu kuona hatima ya mchakato huu na hatua zitakazochukuliwa dhidi ya madai ya uongozi uliovunjwa.

Leave a Comment