ENTERTAINMENT

Kocha Mpya Simba Huyu Hapa

Kocha Mpya Simba Huyu Hapa

Uongozi wa klabu ya Simba umempa mkataba wa miaka miwili aliyekuwa kocha msaidizi wa Raja Casablanca, Fadlu David, ambaye atatua nchini Ijumaa akiwa na wasaidizi wake.

RELATED: CAF Announces Qualifying Draw for AFCON 2025

Kocha David amethibitisha ujio wake Tanzania kupitia ukurasa wake wa Instagram, ambapo aliwaaga viongozi, wachezaji, na mashabiki wa Raja Casablanca kwa maneno haya: “Ulikuwa ni wakati mzuri, msimu mzuri, wachezaji bora, wafanyakazi wenzangu tulikuwa na benchi bora bila kuwasahau mashabiki.”

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Simba kimeliambia Mwanaspoti kuwa kocha David anakuja na wasaidizi wake pamoja na meneja wa timu hiyo. “Ni kweli Simba tulikuwa kwenye mazungumzo na makocha wawili, akiwemo Msauzi, Steve Khomphela, lakini tumeshindwana katika baadhi ya mambo na kuamua kumalizana na David, ambaye amesaini miaka miwili,” kilisema chanzo hicho na kuongeza: “Makubaliano na David ni kuja na wasaidizi wake ambao amewapendekeza mwenyewe. Watatua nchini Ijumaa kwa ajili ya kukamilisha mipango yote na baadaye timu itimkie Misri tayari kwa maandalizi ya msimu mpya.”

Wakati ujio wa kocha huyo mwenye Leseni A ya Caf na wasaidizi wake unatarajiwa, imethibitishwa kuwa kwenye benchi la ufundi la timu hiyo, mchezaji wa zamani na kocha wa muda mrefu, Suleiman Matola, ataendelea kuwepo. Hata hivyo, hatma ya kocha Juma Mgunda bado haijafahamika. “Mgunda alimaliza mkataba na hajasaini mwingine na wala hayupo kwenye safari ya Misri Jumatatu.”

Leave a Comment