Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (Latra) imetangaza nauli za abiria kwa usafiri wa reli ya kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma. Kwa watu wazima, nauli itakuwa Sh 31,000, wakati watoto wa umri chini ya miaka 12 watalipa nusu ya gharama hiyo.
RELATED: Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Tano na Vyuo 2024
Hata hivyo, nauli hizi ni pungufu kidogo ikilinganishwa na nauli za mabasi kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma, ambazo zinatoza kati ya Sh 29,000 na Sh 35,000 kulingana na daraja la basi.
Kwa safari kutoka Dodoma hadi Makutupora, mtu mzima atalipa Sh 37,000, na watoto wa umri chini ya miaka 12 watalipa Sh 18,500.
Nauli hizi zimetangazwa siku chache kabla ya treni hii kuanza safari zake rasmi mwezi Julai mwaka huu, kama ilivyotangazwa awali. Taarifa ya Latra imesema nauli hizi zimepitishwa na Bodi ya Wakurugenzi ya Latra kwa kuzingatia umbali kwa kilomita.
Masharti mengine yaliyotajwa ni kwamba mtoa huduma, Shirika la Reli Tanzania (TRC), lazima awe na leseni ya usafirishaji, ithibati ya usalama wa miundombinu ya reli na mabehewa, na kutumia mfumo wa utoaji tiketi za kielekroniki.
Kwa mujibu wa Latra, nauli kwa watu wazima na watoto zaidi ya miaka 12 ni Sh 9.51 kwa kilomita, wakati watoto wa miaka 4 hadi 12 watalipia Sh 34.76 kwa kilomita. Watoto wenye umri chini ya miaka minne hawatalipa nauli.