Experience the infectious beats and captivating lyrics of “Na Nusu” by Harmonize as you read and sing along. This track stands as yet another testament to Harmonize’s ability to deliver hit songs in East Africa.
RELATED: Jux – Bado LYRICS
Harmonize – Na Nusu Lyrics
Mwanamke ni mtu na nusu
Kukatishwa tamaa usiruhusu
Mwanamke ni mtu na nusu
Kurudishwa nyuma usiruhusu
Na kama mwanaume ndo kichwa cha familia
Basi mwanamke ndo shingo na kiwiliwili
Amani ya mume aliye bora inatengenezwa na mke anapoianza siku
Hata furaha ya mume aliye bora inakamilishwa na mke ifikapo usiku
Yeeeh si ujinga kukubali matokeo oooh
Na sio suala la kupinga wanatuzidi upeo oooh
Ingekuwa hiari yangu mimi ningewapa kila cheo ooooh
Muaadilifu kama mama yangu sijamuona mpaka leo oooh
Samia Suluhu ni mtu na nusu
Mboni Mpaye mpango ni mtu na nusu
Mariam Mwinyi ni mtu na nusu
Mary Majaliwa ni mtu na nusu
Dkt Tulia ni mtu na nusu
Anna Makinda ni mtu na nusu
Bibi Titi ni mtu na nusu
Sophia Kawawa ni mtu na nusu
Pata kucha litazama na lifike kiama
Hutomwona kama mama mama
Mwanamke ni kiumbe jasiri
Ile miezi sita ni siri
Baba asingeweza hata miwili
Hata uwe tajiri tajiri kamwe huwezi kuwa na mama wawili wawili
Mume ataoa wawili
Mwanamke hawezi kuwa na wawili fikiri
Si ujinga kukubali matokeo oooh
Na sio suala la kupinga wanatuzidi upeo oooh
Ingekuwa hiari yangu mimi ningewapa kila cheo ooooh
Muaadilifu kama mama Konde sijamuona mpaka leo oooh
Maria Nyerere ni mtu na nusu
Bi Fatuma Karume ni mtu na nusu
Sitti Mwinyi ni mtu na nusu
Mama Anna Mkapa ni mtu na nusu
Salma Kikwete ni mtu na nusu
Janeth Magufuli ni mtu na nusu
Getrude Mongela ni mtu na nusu
Bi Mwenda ni mtu na nusu
Bi Kidude ni mtu na nusu
Mama Khadija Kopa ni mtu na nusu