Mtangazaji maarufu wa Clouds FM, Gadner G. Habash, aliyefahamika kwa jina la ‘Captain‘, amefariki dunia leo tarehe 20 Aprili 2024.
RELATED: Lava Lava Ft Diamond Platnumz – Kibango (Prod. Mr. LG)
Gadner, ambaye aliipata umaarufu mkubwa kupitia kipindi cha ‘Jahazi’, alikuwa amelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es Salaam kutokana na matatizo ya shinikizo la damu.
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Wasafi Media, ambapo wametoa salamu za rambirambi kwa familia, Clouds Media Group, ndugu, jamaa na marafiki, wakisema: “Tunatoa pole kwa familia, Clouds Media Group, ndugu, jamaa na marafiki. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amin.”