ENTERTAINMENT

Baba Levo Adai Kupigwa na Mkewe, Picha za Majeraha Zasambaa Mtandaoni

Baba Levo Adai Kupigwa na Mkewe

Revokatus Chipando, maarufu kama Baba Levo, ni msanii wa HipHop kutoka Tanzania, chawa, brand ambassador, na mtangazaji katika kituo cha Wasafi FM. Ameingia tena kwenye vichwa vya habari leo tarehe 18 Aprili 2024, baada ya kupost ujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagram akidai kwamba amepigwa na mkewe, Mama Ruby. Baba Levo aliandika: “MAMA RUBY AMENIPIGA 😭😭😭😭😭🙏🏼🙏🏼🙏🏼🙏🏼,” akishirikisha picha iliyomuonesha akiwa na mikwaruzo iliyotokana na chuku kwenye mwili wake.

RELATED: Marioo – Hakuna Matata (Prod. S2kizzy)

Baba Levo na Mama Ruby wamewahi kutengana hapo awali, ambapo Mama Ruby alimpeleka Baba Levo polisi na kumwachia watoto. Kipindi hicho, Baba Levo alianzisha mahusiano na Asma, ambaye alikuwa mchepuko wake. Hata hivyo, baada ya kushawishiwa na marafiki, wawili hao walirudiana na kuanza kuishi pamoja tena. Pamoja na hayo, Baba Levo alimweleza Mama Ruby kwamba hawezi kuachana na mchepuko wake kwani alikuwa msaada mkubwa wakati Mama Ruby alipoondoka.

Wasanii mbalimbali na mashabiki wameonyesha hisia zao kwa kutoa maoni kwenye post ya Baba Levo, wengine wakicheka na wengine wakitoa utani.

RELATED: Marioo na Paula Wanatarajia Mtoto wa Kike, Waandaa Baby Shower

This image has an empty alt attribute; its file name is commetns-1-560x800.png

Mama Ruby na Baba Levo wana watoto wawili, Ruby na Platnumz, na hii si mara yao ya kwanza kuingia katika mzozo wa kifamilia. Miezi michache iliyopita, walikumbwa na mzozo mwingine baada ya Baba Levo kumnunulia mchepuko wake zawadi na kusema kwamba hawezi kuachana naye. Mzozo huo uliisha na Baba Levo kutangaza kwamba ameachana na mchepuko huo.

Leave a Comment