ENTERTAINMENT

Marioo afunguliwa kesi ya Sh. Million 550 kwa kukiuka mkataba

Marioo afunguliwa kesi ya Sh. Million 550 kwa kukiuka mkataba

Msanii maarufu wa Bongo Flava, Omary Mwanga, maarufu kama Marioo, pamoja na meneja wake Sweetbert Mwinula, wamefunguliwa kesi ya madai na Kampuni ya Kismaty.

Wawili hao wanadaiwa kuvunja mkataba uliopangwa kwa Marioo kutumbuiza katika hafla ya Mr & Miss Vyuo Vikuu Kanda ya Kaskazini iliyokuwa ifanyike Septemba 23, 2021. Kampuni ya Kismaty inawadai fidia ya Tsh. 550,000,000 kwa madai ya kutotokea kwenye hafla hiyo kama ilivyokuwa imekubaliwa.

Kesi hii inasubiriwa kusikilizwa katika Mahakama Kuu ya Arusha mbele ya Jaji Joackim Tiganga, tarehe 18 na 19 Machi, 2024.

Leave a Comment