ENTERTAINMENT

Taifa Laomboleza: Rais Mstaafu Ally Hassan Mwinyi Afariki Dunia

Rais Mstaafu Ally Hassan Mwinyi Afariki Dunia

Rais Mstaafu wa Tanzania wa awamu ya pili, Ally Hassan Mwinyi, ameaga dunia Februari 29, 2024, saa 11:30 jioni akiwa anapokea matibabu katika hospitali moja jijini Dar es Salaam kutokana na ugonjwa wa saratani ya mapafu.

Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kifo cha Mzee Mwinyi, ambaye aliiongoza Tanzania kuanzia mwaka 1985 hadi 1995. Alieleza kwamba Mzee Mwinyi alikuwa akipokea matibabu tangu Novemba 2023 huko London, Uingereza, kabla ya kurejea nchini Tanzania kuendelea na matibabu jijini Dar es Salaam.

Kufuatia msiba huu, Rais Samia ameagiza siku saba za maombolezo kuanzia kesho, kuomboleza kifo cha kiongozi huyo mpendwa.

Taifa Laomboleza: Rais Mstaafu Ally Hassan Mwinyi Afariki Dunia

Leave a Comment