NECTA Tangazo Kwa Watahiniwa wa Kujitegemea (CSEE na FTNA) 2024
Katibu Mtendaji, Baraza la Mitihani la Tanzania, anawajulisha watu wote wanaotarajia kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Upimaji wa Kidato cha Pili (FTNA) Novemba 2024 kama Watahiniwa wa Kujitegemea kuwa usajili wao utafuata maelezo yafuatayo:
RELATED: Matokeo Ya Kidato Cha Pili 2023/2024 – NECTA Form Two Results 2023/2024
- Kipindi cha usajili kitaanza tarehe 01/01/2024 na kitahitaji ada ya usajili ya Shilingi 50,000/= kwa wanaojisajili CSEE na Shilingi 10,000/= kwa wanaojisajili FTNA. Usajili utaendelea hadi tarehe 29/02/2024.
- Kwa wale watakaojisajili kwa kuchelewa kuanzia tarehe 01/03/2024 hadi tarehe 31/03/2024, ada ya usajili itakuwa Shilingi 65,000/= kwa Watahiniwa wa Kidato cha Nne (CSEE) na Shilingi 15,000/= kwa Watahiniwa wa Upimaji wa Kidato cha Pili (FTNA), ikiwa ni ada ya kawaida pamoja na faini.
- Watahiniwa wa Kidato cha Nne (CSEE) 2024 ni wale ambao wamerudia Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE), wamefanya na kufaulu Mtihani wa Maarifa (QT) katika kipindi kisichozidi Miaka Kumi (10) iliyopita, au wamefanya na kufaulu Upimaji wa Kidato cha Pili (FTNA) katika kipindi kisichozidi Miaka Kumi (10) iliyopita, au wana sifa zinazolingana na hizo zilizopatikana kutoka nje ya nchi na kufanyiwa ulinganifu na Baraza la Mitihani la Tanzania.
- Watahiniwa wa Upimaji wa Kidato cha Pili (FTNA) ni wale ambao wanatafuta sifa ya kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne kama Watahiniwa wa Kujitegemea.
PAKUA PDF YA TANGAZO LA USAJILI WA WATAHINIWA WA KUJITEGEMEA (CSEE NA FTNA) 2024
Usajili unafanyika kwa njia ya mtandao kwa kufuata hatua zifuatazo:
- Tembelea Kituo unachotarajia kufanyia Mtihani ili kupata maelekezo kutoka kwa Mkuu wa Kituo kuhusu usajili wa Watahiniwa wa Kujitegemea.
- Mkuu wa Kituo cha Watahiniwa wa Kujitegemea atakuingiza kwenye mfumo wa usajili kwa kutoa namba rejea ya Mtahiniwa ili upate ‘Control Number’ ya kufanyia malipo ya ada ya Mtihani.
- Baada ya kupata ‘Control Number’, fanya malipo ya ada ya Mtihani benki kwa kutumia namba hiyo.
- Malipo ya ada ya Mtihani yanaweza kufanywa kupitia Benki ya NMB, CRDB, au NBC.
- Rudi tena kwa Mkuu wa Kituo cha Watahiniwa wa Kujitegemea ili kusajiliwa kwa ajili ya Mtihani unaotarajia kuufanya.
- Hakikisha unakamilisha usajili kwa kuambatanisha vielelezo vyote vinavyohitajika kwenye usajili, kama picha, orodha ya masomo ya kusajiliwa, Kivuli cha cheti cha Kuzaliwa, namba ya simu, na taarifa nyingine muhimu za usajili.
- Baada ya kukamilisha usajili, utapewa nakala moja ya fomu ili iwe kumbukumbu yako, na nakala ya pili itabaki kituoni ambapo nakala ya tatu itapelekwa Baraza la Mitihani.
Kwa maelezo zaidi kuhusu utaratibu wa usajili, tembelea tovuti ya Baraza la Mitihani la Tanzania kwenye www.necta.go.tz. Waombaji wanashauriwa kusajiliwa mapema kwani mfumo wa usajili utafungwa baada ya kipindi cha usajili kumalizika.
Pia, unaweza kupata habari zaidi kuhusu usajili wa watahiniwa wa kujitegemea CSEE na FTNA 2024 kwenye tovuti ya NECTA, na pia kusoma kuhusu usajili wa Kidato cha Sita, matokeo ya Kidato cha Nne na Darasa la Saba, pamoja na taarifa nyingine za NECTA.