ENTERTAINMENT

Dulla Makabila Atoa Wimbo ‘Furaha’ Akimponda Ex-Wake Zaylissa

Dulla Makabila Atoa Wimbo 'Furaha' Akimponda Ex-Wake Zaylissa

Dulla Makabila, msanii maarufu wa muziki wa Singeli nchini Tanzania, ameachia wimbo mpya uitwao “Furaha“, ambao umeonekana kuwa dedication yenye utata kwa aliyekuwa mpenzi wake, Zaylissa. Zaylissa, ambaye hapo awali alikuwa mke wa Dulla Makabila, alitengana naye baada ya ndoa yao kushindikana, hali iliyopelekea Dulla kumpa Zaylissa talaka tatu. Tukio hili liliibua mjadala mkubwa na gumzo katika mitandao ya kijamii.

Miezi sita baada ya kutengana kwao, Zaylissa alijikuta katika mahusiano mapya na Haji Manara, aliyepata umaarufu kama msemaji wa vilabu vikubwa vya soka nchini Tanzania, Simba na Yanga. Jana, kwenye sherehe yao ya kifahari iitwayo ‘The Royal Birthday’, Haji Manara na Zaylissa walivalishana pete ya uchumba, na katika tukio hilo, Manara alimzawadia Zaylissa gari.

DOWNLOAD WIMBO HUO HAPA

Kufuatia matukio haya, Dulla Makabila amejibu kwa kutoa wimbo huu mpya, “Furaha“, ambao unaonekana kumponda Zaylissa. Katika wimbo huo, Dulla anadai kwamba Zaylissa alishindwa kumzalia watoto kwa sababu alitumia dawa za kuzuia mimba (P2), na kuongeza kejeli kwa kusema, “amzailie mzungu”, akimaanisha Haji Manara. Wimbo huu umezua hisia tofauti na mjadala miongoni mwa wafuatiliaji wa muziki wa Singeli na wapenzi wa burudani nchini Tanzania.

Leave a Comment