Habari ya mjini imekuwa kuhusu Diamond Platnumz, msanii maarufu wa Bongo Flava, ambaye ametangaza kupitia insta story yake kwamba kuanzia sasa yeye ni ‘single boy.’ Hii inakuja baada ya tetesi nyingi kuhusu uhusiano wake na msanii wa kike kutoka lebo yake, Zuchu.
- RELATED: Diamond Platnumz Ft Khadija Kopa – Nasema Nawe
- RELATED: Rayvanny Ft Diamond Platnumz – Vumbi (Prod. S2kizzy)
- RELATED: Diamond Platnumz – Jeje (Prod. Kel P)
- RELATED: Zuchu Ft Mbosso – Ashua
Diamond alitumia maneno haya: “From Today on ningependa niwatangazie rasmi kuwa I AM SINGLE, sidate wala sina mahusiano na mwanamke yoyote.” Hii ni baada ya mama yake Diamond, Bi. Dangote, kukanusha uvumi uliokuwa ukienea kuhusu uhusiano wa kimapenzi kati ya Diamond na Zuchu.
Mambo yamechukua mkondo mwingine baada ya Mange Kimambi, maarufu kama ‘dada wa Taifa,’ kutoa maoni yake. Mange ameonekana kufurahishwa na kuvunjika kwa mahusiano ya Diamond na Zuchu, akisema kuwa Zuchu alikuwa akimroga Diamond ili aweze kumpenda. Mange amemsihi Diamond asirudi kwa Zuchu, akisema kwamba Zuchu hawezi kuwa katika mahusiano ya kudumu na mtoto wa mama Dangote.
Mange ameenda mbali zaidi kwa kusema kwamba atampa Diamond mwanamke mwenye hadhi, tofauti na Zuchu ambaye anadaiwa kutokuwa na mvuto. Mwisho, Mange ametoa onyo kwa Diamond kuhusu kusoma dua ili kuepuka urogi wa Zuchu na mama yake.
Hii ni moja ya sakata za kimapenzi zinazozidi kuchukua nafasi kubwa katika ulimwengu wa burudani Tanzania, na mashabiki wanasubiri kwa hamu kuona itakavyoendelea.