ENTERTAINMENT

Baba Levo na Mwijaku ni Maadui Zangu Mpaka Kifo – Dotto Magari

Baba Levo na Mwijaku ni Maadui Zangu Mpaka Kifo - Dotto Magari

Dotto Magari, ambaye amejizolea umaarufu mkubwa kwenye mitandao ya kijamii, amesisitiza kuwa yeye si “chawa” bali ni influencer.

Katika mahojiano yake na Wasafi Fm kwenye kipindi cha Fresh Weekend, Dotto alijadili suala la Baba Levo na Mwijaku, akieleza kuwa wao ni maadui zake na kwamba hawajachangia lolote katika mafanikio yake kwenye tasnia ya sanaa hapa bongo.

Dotto anasisitiza kuwa mafanikio yake yametokana na juhudi zake binafsi na kujituma kwake katika kazi zake za uinfluencer.

Leave a Comment