Mbaazi ni mimea yenye mizizi mirefu inayopendelea mazingira yenye joto, kati ya nyuzi joto 25 hadi 40 Celsius. Haifai sana kwa mazingira yenye baridi, hivyo ni muhimu kuchagua kipindi sahihi cha kupanda kulingana na mazingira yako. Katika maeneo mengi ya Tanzania yenye joto, mbaazi hukua vizuri. Inaweza kuchanganywa na mazao kama ulezi, mtama, mahindi, au maharage.
- RELATED: Rayvanny – Woza Ft. Diamond Platnumz (Prod. Trone)
- RELATED: Lava Lava Ft Diamond Platnumz – Bado Sana (Prod. Mr LG)
- RELATED: Baba Levo Ft Diamond Platnumz – Shusha
- RELATED: Diamond Platnumz – Number One Remix Ft Davido
- RELATED: Diamond Platnumz Ft Khadija Kopa – Nasema Nawe
Table of Contents
Nafasi ya Upandaji
Panda kwa nafasi ya mita 1 kwa 1.5, kutoka mche hadi mche 1m, na mstari hadi mstari 1.5m. Unaweza pia kuchanganya na mazao mengine katika nafasi hii.
Muda wa Kuota Mbegu
Mbali na muda wa siku 4 hadi 21 baada ya kupanda mbegu hadi kuota, hakikisha unazuia magugu mapema.
Muda wa Kukomaa
Mbaazi huchukua siku 60 hadi 80 kutoka kupanda hadi kutoa maua, na baada ya hapo siku 50-75 zaidi kutengeneza mbegu zilizokomaa. Jumla, zinaweza kuchukua kati ya miezi 5 hadi 6 kukomaa.
Idadi ya Mbegu kwa Eka
Unahitaji kilo 10 za mbegu kwa ekari moja ikiwa unapanda mbegu mbili kwa shimo, au kilo 5 kwa ekari kama unapanda mbegu moja kwa shimo.
Wadudu Waharibifu na Udhibiti
- Funza wa matunda
- Funza wa kukata mimea michanga
- Mnyauko (Fusarium Wilt)
- Ukungu-Fangasi
Tumia dawa kama Karate, Match, Phyrinex, uduall, au Seecron. Lita 3 za dawa zinatosha. Kuzuia ukungu, tumia dawa kama Ridomil Gold, Ebony, Ivory, au Nordox, ambapo lita mbili au kilo mbili za dawa zitatosha.
Mbolea za Kupandia
Tumia mbolea kama Yara Mila Winner, NPK, DAP, Minjingu, au TSP. Mifuko miwili kwa ekari inatosha.
Wakati wa Kukuzia
Utahitaji mbolea kama CAN, UREA, NPK, au Yara Mila Winner. Mifuko mitatu itatosha kwa ekari moja.
Mavuno
Unaweza kuvuna kati ya tani 1 hadi 4 kwa ekari, yaani gunia 10 hadi 40 za uzito wa kilo 100, kulingana na rutuba ya ardhi yako.