NEWS

Lori la Mafuta Laanguka Segera Tanga, Wananchi Wachota Mafuta

Lori la Mafuta Laanguka Segera Tanga

Lori lililobeba shehena ya Mafuta ya Petroli limepata ajali na kuanguka katika eneo la segera Wilayani Handeni mkoani Tanga.

RELATED: Paula Kajala ajibu madai ya kupokonywa gari na Harmonize

Baadhi ya wakazi wa Segera walijitokeza na kuanza kuchota mafuta, hata hivyo muda mfupi baadaye polisi wamefika eneo hilo na kuwatawanya wananchi hao na hivyo kuepusha ajali ambayo ingetokea endapo moto ungewaka katika eneo hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Handeni Bi. Siriel Mchembe ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya ya Handeni amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo

“Nalipongeza Jeshi la Polisi Handeni kwa kufanikiwa kudhibiti wananchi waliokuwa wanachota mafuta kwenye Gari la mafuta ya petrol lililopata ajali Segera. Hakika Mungu awabariki, wananchi chondechonde tusirudie tenaaaaaa!” – DC

Leave a Comment