Baada ya video fupi kusambaa jana ikionesha Askari Polisi wakizozana na Walinzi/Wafanyakazi wa barabara ya Mabasi ya mwendokasi, Jeshi la Polisi limetoa onyo kali na kusisitiza kuwa barabara hiyo ni kwa ajili ya Mabasi ya Mwendokasi tu na hakuna chombo kingine chochote kinatakiwa kuitumia.
RELATED: Msimamo Ligi kuu Bara Tanzania | NBC Standings 2022/2023
Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi SACP David Misime imesema barabara hiyo haitakiwi kutumiwa na chombo kingine chochote isipokuwa Mabasi ya mwendokasi pekee.
“Si kwa Raia wala kwa Mtu yeyote, mwenye cheo cha aina yoyote awe anaendesha mwenyewe au anaendeshwa anayeruhusiwa kupita katika Barabara za Mwendokasi”
kwa Taarifa zaidi unaweza ukabonyeza play kufahamu zaidi.