ENTERTAINMENT SPORTS

Kocha Wa Yanga Aumizwa na Adhabu ya Benard Morrison

KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi ameshtushwa sana kusikia kwamba winga wake kutoka Ghana, Bernard Morrison ‘BM33’ atakosa mechi tatu za Ligi Kuu Bara na kuwaka akiwa Ulaya alikoenda kwa dharura wakati ligi ikiwa imesimama kupisha mechi za kimataifa kwa kalenda ya FIFA.

Akizungumza kutoka Ubelgiji alipo, Nabi alisema adhabu hiyo ilimshtua kwani alipata taarifa hizo akiwa mezani na familia yake na kuharibu furaha yake yote.

Nilipata hizo taarifa bahati mbaya zilinikuta nikiwa mezani na familia, ziliniumiza sana huu ni wakati ambao kwa mechi zilizo mbele yetu kocha yoyote angependa kuwa na wachezaji wake wote. Kuna kitu ambacho huwa kinanishtua sana naona kama timu yangu inaandamwa sana, wachezaji wangu wanaumizwa sana lakini kwa kiasi kikubwa huwa sioni sana maamuzi kama haya yakifanyika, nimeamua kuwaachia viongozi hili nitaendelea na majukumu yangu uwanjani.” alisema Nabi.

Also, check more tracks from Diamond Platnumz;

Kwa Video Zaidi za Habari na Burudani Usiache Ku Subscribe Channel yetu ya Youtube @CitiMuzik TV

Leave a Comment