Staa wa Simba SC, Clotous Chota Chama ameshinda tuzo ya Emirate Alluminium Profile ya mchezaji bora wa mwezi August wa Simba SC pamoja na Tsh milioni 2 Chama ametwaa tuzo hiyo akiwashinda Sadio Kanoute na Pape Sakho.
RELATED: Msimamo Ligi kuu Bara Tanzania | NBC Standings 2022/2023
Chama amekuwa mchezaji bora wa August 2022 Kutokana na kufanya vizuri zaidi kiasi cha kuwateka mashabiki wa Simba SC na kuamua kumpigia kura yeye mbele Sadio Kanoute na Pape Ousmane Sakho.
Chama ndani ya mwezi August akiwa Simba SC amecheza jumla ya mechi nne ambapo amefunga magoli matatu, mechi alizocheza Chama ni mchezo dhidi ya Geita Gold, Kagera Sugar na michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana na Al Hilal Omdurman.