Moja kati ya vitu ambavyo huwezi Kuvi control pale unaokuwa maarufu ni maneno ya watu,wazungu wana msemo wao kuwa ‘when you are on top you became a topic’ yani unapokuwa juu maisha yako yanakuwa ni mada kwenye vinywa vya watu kwa hiyo chochote unachofanya watu wanakitazma na kukiongelea.Watu wataongea story nzuri na mbaya kuhusu wewe bila kujali unajisikiaje na kwa watu maarufu huwa tunaziita Skendo.
Saasa leo nimekuandalia makala maalum kuhusu SKENDO 10 zinazomkabili Msanii Diamond Platnumz.
Naseeb Abdul Juma Isaac Au Diamond Platnumz ni moja ya wasanii wakubwa Barani Afrika na kwa Tanzania tunaamini kuwa ndiye msanii namba moja kwa sasa.Kwa kusema hayo inamaanisha kuwa yeye ndiye msanii anyefuatiliwa zaiddi kuliko msanii yeyot yule na pengine ndiye msanii mwenye skendo nyingi kwenye vichwa vya habari.
Zifuatazo ni baadhi ya skendo ambazo staa huyo amekutana nazo (Endelea kufuatilia kupitia Video hapo chini)