Dizasta Vina – Shahidi Lyrics
Ah
Nilipanda kwenye jukwaa, watu walinishangaa
Unadhifu wa meli haukufanana na nilivyovaa
Kabla sijatoa salamu, walipoteza hamu
Ya kuburudika wengine wakaanza kusambaa
Nilikuwa na nywele nyingi zilionyesha pia siku ni nyingi tangu mara ya mwisho ziwekwe maji
Wale Matajiri waliosheheni kwenye viti walicheka wakihisi mi’ chizi au mchekeshaji
Walio karibu pia wakaanza kun’tunza pesa
Na walio mbali walijaribu kurusha fedha
Kwa yote niliyowaeleza hakuna alieyaweka kichwani
Wote walihisi kuwa nataka kuchekesha
Walinitemea shombo kwa kejeli
Wengine walihisi nalianzisha zogo kwenye meli
Mwonekano haukuyabeba maneno yangu
Hawakuamini niliposema kuwa chombo kina mushkeli
Niliwaeleza kuwa kule ndani kuna tundu dogo
Linapitisha maji linazamisha chombo
Waliendelea kujadili siasa na vibonzo
Hakuna aliyejadili kuhusu roho
Za wasakatonge wanyonge wasafiri daraja la tatu
Hawakulipa pesa nyingi ila walikuwa ni watu
Maji yalianza kuingia vyumbani mwao
Iliwekwa mipaka hivyo taarifa hazikufika katu
Nilienda mpaka chumba cha sauti
Nitoe tangazo kabla hatujakumbwa na mauti
Mtoa sauti aliwataja matajiri
Akiwapa sifa majina makubwa na saluti
Niliwaambia wekeni glasi chini mtege masikio
Hizo kelele mnazosikia si sherehe ni vilio
Wakasema nimedata nataka kuanzisha vagi
Ilionyesha wazi hawakuona mbeleni tishio
Hata kwenye vyumba vya wasomi maarufu
Vyeti walihodhi maradufu
Niliwahoji kuhusu ubovu wa meli wengi
Waliujua ubovu lakini walisema haiwahusu
Naapa haki nilienda kote..
Nilihamaki kuona wote wamepewa cocktail
Walikunywa na kula bata, walikunywa hata
Mziki waliruka mpaka mafundi walilewa pombe
Wakasema huyu ni mjinga hajielewi
Kisha wakanituhumu mi’ ni mlevi wakati
Wamelewa wao, wakanipa matusi ya kienyeji
Hawakutaka kusikiliza hata semi
Nilimwona nahodha nikahisi nimeipata nafuu
Alikua kando ya mrembo fulani hivi daraja la juu
Gauni refu mwili mzima amepakaza tatuu
Aliponiona aliendelea kuikata tamboo
Kweli starehe inaweza kukufanya hauoni
Kukufanya hauoni
Kwani licha ya kujua nipo hapo kutoa
Taarifa nahonda na mrembo waliendelea kushikana maungoni
Nahodha akaipaza miguno, akinipuuza
Mrembo naye akafata mkumbo
Nahodha akachukua chupa akakata mafundo
Wakaendelea kupapasana mifumo
Ya viungo vyao vya uzazi walikuwa radhi kuzika shift
Hawakusikia chochote nilichosema
Nakumbuka mrembo alidiriki kuniita mwizi
Nikafatwa nikaja kupigwa na walinzi
Wenzangu waliogundua ubovu wa chombo walihofu
Wakaamka wakawahi kubeba vyombo vya wokovu
Walikaa kimya kwa sababu tu ya ubinafsi
Mi’ nikabaki ili niziokoe roho za wachovu
Ilikuwa bahati mbaya hakuna aliyesadiki
Mshereheshaji akaongeza sauti kubwa ya mziki
Kiasi sauti yangu ikaanza kuwa haisikiki
Walinzi walitumwa wanidhibiti
Nilifungwa kwenye chumba chenye giza chini nisihame
Nikachapwa mijeledi thelathini na minane
Nikapambana nikatoroka na mtumbwi kwenda kando
Usalama wangu ulianza hapo
Nilishuhudia kila inchi ya ile meli ikizama
Roho za kila mkwezi zikihama
Kutoka uhai kwenda kifo, sikufurahi kuona hivyo
Ila sikuwa na jambo ningeweza ‘fanya
Wakati walokole wakiombea kupona
Tajiri na maskini waligombea maboya
Wanazi walionicheka wakasema mi’ ni zuzu
Walikufa wote hata walionisema kinoma
Ahadi ya maisha mapya ilisemwa ila hakuna aliyekumbuka
Pesa zilizagaa na hazikuguswa
Hata wale waumini walioitamani mbingu
Na kuisifu, kumbe wote waliogopa kufa
Waliokuwa wanajikweza na ukubwa na ubosi mwingi
Yaliwaishia majivuni
Njia walizibuni, waliua mpaka wenza ili ‘kufosi kingi’
Kifo kiliwatia mbavuni
Walikufa wengi kama kuku kote walizagaa
Hata wanajeshi waliozijua ‘kareti’
‘Walidedi’ maana ujuzi wa mitutu haukufaa
Mbele ya kufa hakuna mwenye nguvu au shujaa
Nilishuhudia makafiri wakiungama
Masikini na Matajiri waligusana
Utu uliwatoka uasi ulisogea
Tofauti za kabila na rangi zilipotea
Watu wenye bendi na ‘tisheti’ zao za kijani
Walisahau kuwa nao pia wapo ndani
Milango ilokuwa wazi yote ilijifunga
Walipiga kelele na mwisho walikufa maji
Washairi waswahili na tashtiti zao
Matajiri na masikini wote chini yao
Kwaya hazikutoa sauti ndimi zao
Walikufa wote mpaka mahujaji na dini zao
Wakati wa kufa hakuna dawa
Hakuna kiongozi hakuna chawa
Hakuna tofauti ya mali na milki zetu
Kwenye kufa hata wenye nacho na wasio nacho wanakuwa sawa
Hazikusaidia diplomasia za digitali
Asili ilihakikisha walosalia hawafiki mbali
Waliendelea kungoja msaada kwa tumaini
Mwisho wote walikufa sababu ya baridi kali
Walikufa makini sababu ya wapuuzi wachache
Walofanyia uzembe tangazo langu
Wamiliki walikula bima wakasingizia ajali
Ilihali meli ilizama mbele ya macho yangu… ah!
Viongozi hawakubebwa na vyeo vyao
Maana wote walikuwa mbali na ridhaa
Niliona kofia za ufalme zikielea kando yao
Ila hakuna aliyekuwa hai kuzivaa
Niliwapa taarifa lakini wakanitwika maudhi
Waliishia kulia na hazikusikika sauti
Walipambana Mwisho yaliwafika mauti
Nilibaki hai kuziandika sarufi