Zabron Singers – Sweetie Sweetie! LYRICS
Hatimaye ni leo, ni siku yetu
Siku yetu muhimu, harusi yetu
Uwepo wenu nyote hehee
Kwetu ni kitu
Kwetu ninyi ni ndugu
Leo na kesho
Harusi maua
Ng’ari ng’ari wanapendeza
Leo ni furaha shangwe na furaha
Harusi maua hee
Tabasamu suti na shela
Wacha tufurahi, sote tufurahi
Sweetie, sweetie, sweetie
Haikuwa rahisi
Tufike leo hii
Na hapa tulipo
Ndio siku yetu uuh
Ipo muhimu uuh
Ya harusi
Sweetie, sweetie baby
Haikuwa rahisi
Tufike eeh leo hii
Na hapa tulipo
Ndio siku yetu uuh
Ipo muhimu uuh
Ya harusi
Sasa nyumba moja, mwili mmoja
Kila kitu ni moja, tuwe pamoja
Upendo naongeza, nawe ongeza
Heshima napandisha, tuwe pamoja
Sweetie, sweetie baby
Haikuwa rahisi
Tufike eeh leo hii
Sasa wewe ni mimi
Mimi ni wewe
We ndo mwandani wangu
Rafiki yangu
Sasa wewe ni mimi
Mimi ni wewe
We ndo mwandani wangu
Rafiki yangu
Na wazazi wameona, wakaturuhusu
Kwa furaha wakasema hee
Tumewabariki
Na mwenyezi Maulana
Atatubariki
Tukazae na tulee hehee
Watoto wazuri
Sasa wewe ni mimi
Mimi ni wewe
We ndo mwandani wangu
Rafiki yangu
Sweetie, sweetie, sweetie
Haikuwa rahisi
Tufike leo hii
Na hapa tulipo
Ndio siku yetu uuh
Ipo muhimu uuh
Ya harusi
Sweetie, sweetie baby
Haikuwa rahisi
Tufike eeh leo hii
Na hapa tulipo
Ndio siku yetu uuh
Ipo muhimu uuh
Ya harusi
Sasa nyumba moja, mwili mmoja
Kila kitu ni moja, tuwe pamoja
Upendo naongeza, nawe ongeza
Heshima napandisha, tuwe pamoja
Sweetie, sweetie, sweetie
Haikuwa rahisi
Tufike leo hii
Ya ndoa mengi mengi, tupande nayo
Sweetie nikuheshimu, uniheshimu
Mahaba moto moto, yawe ni wimbo
Kwetu yawe waridi, yakanukie
Walikuwepo, walitamani
Nao wakafunga harusi, wakapalangana
Haikuwezekanaa
Kama si Mungu, tusingefika hapa
Na kufurahi hivi
Na leo ni leo mambo sasa ni mambo
Sweetie, sweetie, sweetie
Haikuwa rahisi
Tufike hee leo hii
Na hapa tulipo
Ndio siku yetu uuh
Ipo muhimu uuh
Ya harusi
Sweetie, sweetie baby
Haikuwa rahisi
Tufike eeh leo hii
Na hapa tulipo
Ndio siku yetu uuh
Ipo muhimu uuh
Ya harusi
Sasa nyumba moja, mwili mmoja
Kila kitu ni moja, tuwe pamoja
Upendo naongeza, nawe ongeza
Heshima napandisha, tuwe pamoja
Na tutakumbushana, kukaa na Mungu
Familia ya Mungu, hujaa upendo
Wema kwa ndugu wote wa pande zote
Tutapendwa na wote hata na Mungu
Also, check more tracks from Zabron Singers;