ENTERTAINMENT

Wema Sepetu awakosoa wasioridhishwa na kazi zake

Wema Sepetu awakosoa wasioridhishwa na kazi zake (+VIDEO)
Wema Sepetu awakosoa wasioridhishwa na kazi zake

Mwanamitindo wa Tanzania na muigizaji mashuhuri kutoka Tanzania, Wema Sepetu amewapiga vijembe wanaopeleleza maisha yake kisha kusema mabaya kumhusu.

RELATED: Hamisa Mobetto amkana Rick Ross

Wengi wanafahamu Wema Sepetu kama mpenzi wa zamani wa Diamond Platnumz ambaye waliishi naye kwa mahusiano kwa muda mrefu, lakini mahusiano hayo hayakudumu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Wema ameeleza kwamba amekuwa anashindwa nini husumbua baadhi ya wanamitandao ambao humtupia ya kumkejeli kila siku.

“Yaani binadamu bwana, usipofanye wanasema , ukifanya pia wanasema…sasa sijui hata nifanye nini…Hebu mniache..maana nimechoka kiukweli”

Wema Sepetu awakosoa wasioridhishwa na kazi zake

Wema amesema hayo baada ya kuchokeshwa na maneno hasi ya wanamitandao ambao wamekuwa wakimkejeli kwa kile wanachosema ni ukosefu wa msimamo wa kimahusiano.

RELATED: Nandy azungumzia madai ya kuwa na ujauzito wa Billnass (+Video)

Miezi michache iliyopita Mwanamtindo huyo alipuuzilia mbali madai ya wanamitandao kwamba yuko kwenye mahusiano mengine kwa sasa.

Also, check more tracks from Zuchu;

Leave a Comment