ENTERTAINMENT

Nataka nipate mume mzungu na mwenye pesa nyingi – Rose Muhando

Nataka nipate mume mzungu na mwenye pesa nyingi - Rose Muhando

Wiki jana msanii wa nyimbo za injili kutoka Tanzania Rose Muhando alivuma Mitandaoni baada ya kutangaza kwamba ana mtaka mzungu tajiri ili awe mume wake.

RELATED: Rose Muhando – Ombi Langu

Akiwa kwenye mahojiano na wanahabari msanii huyo aliweka wazi kile alichokuwa anamaanisha na kusema kwamba anamtaka mzungu tajiri.

“Ndoa ni kitu ambacho unajaliwa, siwezi enda kuitafuta au kulima shambani siwezi enda kumtafuta mwanamume, huo ni umalaya, ila nitamwambia mungu,” Muhando alisema.

Aidha msanii huyo alisema kwamba kumchagua mzungu ni chaguo lake, na wala sio mzungu ngozi bali mwenye hela.

“Choice yangu, nimechagua choice yangu. Mbona mzungu anaoa Maasai? Sijaomba mzungu ngozi, nimeambia mungu nipe mzungu mwenye pesa. Si anioe, anipe hizo pesa nikahubiri injili.

RELATED: Rose Muhando Ft Ringtone – Walionicheka (Prod. Teddy B)

Si azeeke kisha anampa Mbwa hela, alete hapa. Kwani nimevunja sheria ya nchi? Kati ya Amri kumi za mungu nimekosea ipi? Basi hiyo imeisha.”

Also, check more tracks from Rose Muhando;

Leave a Comment