Siku ya Jumanne wiki hii kumekuwa na tetesi kemkem ambazo zilisambaa kwa kasi kama moto wa karatasi kwenye ulingo wa burudani kwamba Rayvanny na Paula Kajala kaachana.
RELATED: Nataka nipate mume mzungu na mwenye pesa nyingi – Rose Muhando
Baba Levo kupitia kituo kimoja cha runinga nchini Tanzania amedai kwamba alimuonya Ravyaan kutomlipia karo Kajala kwenda kusoma nchi za ng’ambo.
“Niseme moja kati ya vitu vimetrendi sana..ni Ravyaan na Mchumba wake Paula Kajala, naona kama taa nyekundu imewaka. Ravyaan aliniambia anamlipia ada .Mchumba hasomeshwi,” alisema Baba Levo.
Aliendelea kueleza kuwa, “Mabinti wengi wamezoea kula hela za watu halafu wanawakataa..hata kwa mabaha, ngumi nyingi hutokea kwa sababu hiyo,Mwanamke anaenda analewa pombe ya mtu kisha anatoroka,”
Alipoulizwa kwa nini amesema hayo kuhusu mchumba wa Rayvanny, alidokeza kwamba Ravyanny na kajala ni marafiki wakubwa kwenye mtandao wa kijamii.
RELATED: Khadija Kopa afunguka juu ya penzi la Diamond na bintiye Zuchu
“Wote ninawafuatilia kama jamaa zangu na marafiki zangu, nimeenda kwenye kurasa zao za mitandao wote wameacha kufuatiliana” alidokeza Baba Levo.
Na kweli penye moshi hapakosi moto na tunachosubiria nikuona kama watazungumzia mahusiano yao.
Mchumba hasomeshwi – Baba Levo amchana Rayvanny kuhusu Paula (+Video)
Also, check more tracks from Rayvanny;