ENTERTAINMENT

Khadija Kopa afunguka juu ya penzi la Diamond na bintiye Zuchu

Khadija Kopa afunguka juu ya penzi la Diamond na bintiye Zuchu

Mwanamuziki wa taarab kutoka Tanzania Khadija Kopa ambaye ni mamake mzazi mwimbaji mashuhuri Zuchu, amejibu madai kwenye mitandao ya kijamii kuwa Zuchu anauhusiano wa kimapenzi na staa wa bongo Diamond Platinumz.

RELATED: Zuchu Ft Mbosso – Ashua (Prod. Mocco)

Hivi majuzi, habari za Diamond Platnumz kuwa na mahausiano na Zuchu zilitamba kwenye mitandao ya kijamii na kwenye vyombo vya habari.

Kutokana na habari hizo, kituo kimoja nchini Tanzania kilimhoji mama wa Zuchu,Khadija Kopa kubaini ikiwa yanayosemwa ni kweli ama porojo tu.

Katika mahojiano hayo,Khadija alisema hajasikia watu hao wanauhusiano wa kimapenzi na hata wao wenyewe hawalizungumzia suala hilo. Ila aliwaomba wanahabari wahoji na kusakura pia kubaini ukweli kama upo.

RELATED: Diamond Platnumz – Unachezaje (Prod. S2kizzy)

Kulingana naye watu ambao wanapaswa kuulizwa kama wanamahusiano ni wale wanaohusishwa na mapenzi.

“Naomba muulize Diamond na Zuchu sijui kwa sababu suala zima halinihusu…waulize watu wawili wanaohusika. ikiwa wanachumbiana basi hakuna shinda mradi wao wenyewe wanapendana, “alisema Kopa

Aliongeza kwamba suala la ndoa ni baina ya watu wawili kukaa pamoja na kukubaliana wanavyotaka kuishi.

RELATED: Zuchu reveals that she is in a relationship, as she brags about a gift from bae

“Unaweza kujua ikiwa mwanamume ana kiwango fulani ikiwa unaishi naye?. Hata kama ningemchukulia kila mwanamume usoni basi nisingeolewa na yule niliyenae. Ningeolewa na wa kiwango changu. Unapoishi nao unajifunza zaidi. Zuchu hajaniambia chochote kuhusu uhusiano huo.” Mama mzazi alidokeza.

Khadija Kopa afunguka juu ya penzi la Diamond na bintiye Zuchu (+VIDEO)

Mhariri Davis Ojiambo

Also, check more tracks from Zuchu;

Leave a Comment