Mwigizaji maarufu nchini Marekani, Julia Fox amejitokeza na kueleza bayana kuhusu mahusiano yao kati yake na Muimbaji na Bilionea, Kanye West huku akiweza kwamba kwama ni kweli anampenda sana rapa huyo.
RELATED: Khadija Kopa afunguka juu ya penzi la Diamond na bintiye Zuchu
Hivi majuzi kumekuwa na habari kwenye mitandao ya kijamii kwamba Julie anatamani tu pesa na mali za Kanye West na hana mapenzi ya kweli kwa Bilionea huyo.
Baada ya uvumi huo, Bi Julia Fox alisema kwamba wala hatamani pesa za mwanamuziki huyo ila mapenzi anayompa yanamtosha na kukiri kama ni pesa amewai kuwa kwenye mahusiano na watu walio na pesa kumliko Kanye West.
“Watu wamekuwa wakisema mimi niko na Kanye West kwa kuwa nataka kutengeneza pesa kwa sababu yeye ni milionaire. Wakati mwingine watu wanasema ni mbinu yangu ya kutengenza kiki lakini siko hivo kama ni pesa nimekaa na watu wenya pesa kumshinda Kanye,” alisema Julia Fox.
Kanye West ambaye walikosana na kuachana na Mama wa watoto wake, Kim Kardashian miezi michache iliyopita walijikuta tena katika mvutano mkubwa baada ya Kardashian kumficha Baba wa mtoto eneo ambalo sherehe za kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa bintiye Chicago ilikuwa ikifanyika na baadaye rafiki yake alimjulisha walikokuwa.
RELATED: Kucheatiwa kunauma sana – Jacquline Wolper afunguka
Kutokana na ukaribu wa Kanye west na Julia Fox wanamitandao wamekuwa wakisema ni njia ya kufanya Kim kusikia vibaya.