Msanii maarufu Ibraah kutoka lebo ya Konde Music Worldwide hatimaye amedhibitisha kukamilika kwa albamu yake. Ibraah kwa muda sasa amekuwa akizungumzia ujio wa albamu hiyo ambayo itakuwa ya kwanza kabisa kutoka kwake tangu aanze muziki.
RELATED: Harmonize – Mdomo Ft Ibrah (Prod. Abbah)
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Ibraah aliwaomba mashabiki wake usaidizi katika kuchagua jina la albamu hiyo. Alisema kuwa yeye mwenyewe ashapata jina la kuipa albamu ila angependa kusikia mapendekezo ya mashabiki wake.
Ibraah, hata hivyo, hakufichua habari zaidi kuhusu albamu hiyo. Hakutaja idadi ya ngoma zilizomo kwenye albamu hiyo wala wahusika waliochangia katika utengenezaji wake. Vile vile, hakufichua tarehe kamili ambayo albamu hiyo itatoka.
“Mimi binafsi nimesha pata jina la #Album Ila kwa kuwa naamini bila wewe shabiki yangu mimi sio chochote nakupa nafasi ya pendekezo lako ungependa albam Tuipejina gani ? Nasubiri comment yako,” chapisho la Ibraah mtandaoni lilisomeka.
Ujumbe huo uliibua furaha miongoni mwa mashabiki wake sugu ambao wamekua wakisubiri albamu hiyo kwa hamu na ghamu.
Takriban mwezi mmoja uliopita, Ibraah aliachia ngoma ya ‘Addiction’ ambayo imepokelewa vizuri mno na kufikia sasa imetazamwa takriban mara laki nane.
RELATED: Killy Ft Harmonize – Ni wewe (Prod. Hunter)
Nyimbo anazotoa Ibraah zimekua zikipata mafanikio makubwa na kuna matumaini kuwa msanii huyo atapata heshima kubwa kutokana na albamu yake. Ujio wa albamu ya Ibraah unakuja miezi kadhaa baada ya Harmonize kuachia albamu yake ya pili ya ‘High School’.
Also, check more tracks from Harmonize;
twakupenda huku kenya