Watu kumi mashuhuri waliouawa kwa kupigwa risasi
- JOHN F KENNEDY (JFK)
Alikuwa raisi wa 35 wa marekani aliuwa November 22 mwaka 1963 akiwa raisi wa nne kuuawa kwa kupigwa risasi katika historia ya marekani.
Akiwa na mkewe, kwenye gari la wazi akitoka kwenye hotuba Alipigwa risasi tatu. Mpaka leo hakuna jibu la moja kwa moja juu ya nani aliyehusika kumuua JFK japokuwa Lee Harvey Oswald ndiye aliehusishwa na mauaji hayo.
Lee Harvey Oswald nae aliuawa na raia mmoja (Jack Ruby) siku mbili tu baadae alipokuwa akipelekwa rumande.
Cha ajabu ni kwamba, John kennedy, Lee Harvey Oswald, na raia aliyemuua Oswald, wote walifia katika hospitali ya Parkland Memorial Hospital kwa nyakati tofauti.
Mdogo wa JFK aliyeitwa Robert F. Kennedy nae aliuawa mwaka 1968 (alikuwa anawania uraisi wa marekani)
RELATED: Mambo Kumi 10 Usiyoyajua Kuhusu Adolf Hitler
2. MARTIN LUTHER KING JR
Anafahamika kwa harakati zake za kutetea usawa miongoni mwa waamerika weusi. Martin Ruther king ambaye alitumia dini yake ya kikristo kukemea ukandamizwaji wa watu weusi, aliuawa miaka mitatu baada ya mwanaharakati mwingine Malcom X (yeye alitumia dini yake ya kiislam) Kuuawa mwaka 1965 wote wawili waliuawa wakiwa na miaka 39!
Robert F Kennedy aliyekuwa Mdogo wa raisi wa marekani (John kennedy), na Mgombea wa uraisi, alitoa hotuba ya kukemea vikali mauaji ya Martin Luther King Jr, cha kushangaza nae aliuwa miezi kadhaa baadae!
3. ABRAHAM LINCOLN
Alikuwa raisi wa 16 wa marekani na ndiye raisi wa kwanza wa marekani kuuawa akiwa madarakani. Aliuawa mwaka 1865 na John Wilkes Booth aliyeudhiwa na maamuzi ya Lincoln ya kutambua haki za watu Weusi. Alimuua Lincoln kwenye maonyesho ya muziki.
Booth nae aliuawa siku mbili baadae baada ya jaribio la kutoroka kushindikana.
4. BENAZIR BHUTTO
Alikuwa waziri mkuu wa 11 wa Pakistani na kiongozi wa chama chenye ushawishi mkubwa cha PPP. Alikuwa mwanamke wa kwanza kuongoza taifa la kiarabu akichagizwa na siasa zake safi za kidemokrasia.
Aliuawa disemba 27 mwaka 2007 akiwa kwenye gari yake Ya land cruiser akitoka kwenye mkutano wa kampeni. Gari hilo lililokuwa wazi juu, lilikuwa na uwezo wa kuzuia risasi lakini Bi Bhutto alisimama ili kuwaungia mkono wafuasi wake ndipo alipopigwa risasi an baadae mlipuko kutokea na kuua watu wengine 20 katika eneo la tukio.
5. MAHATMA GANDHI
Pia anafahamiak kwa jina la Mohandas Karamchand Gandhi , Ni maarufu kwa hotuba na kauli zake zinazotumiwa mpaka leo.
Huyu ni kiongozi maarufu zaidi wa India iliyokuwa ikitawaliwa na Waingereza Mahatma gandhi alikuwa kiongozi wa kiroho na kisiasa aliuwa tarehe 30 Januari 1948 na mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu (Nathuram Godse) alipokuwa akielekea kufanya ibada.
6. JOHN LENNON
Nani halijui Kundi la vijana watanashati la The bittles? (kibongo-bongo “bitozi”) lilotamba miaka ya 70 na 80. J.Lenon alikuwa mmoja wa waanzilishi wa kundi hilo lililotamba sana na alifariki tarehe 8 disemba mwaka 1980.
Akiwa anaingia hotelin, Lenon alisikia sauti ikimuita na alipogeuka, alipigwa risasi nne na kupoteza maisha. Baada ya mauaji hayo, muuaji Mark David Chapman aliiachia silaha na kukaa barabarani akisubiri akamatwe! Alihukumiwa kifungo cha maisha na yuko jela mpaka sasa.
7. MALCOM X
Kama ilivyo kwa luther King Jr, Malcom X nae alikuwa mwanaharakati aliyepigania haki za watu weusi.
Alikuwa waziri kwa wakati huo na aliuawa mwaka 1965 baada ya kuamua kuwa Muislam wa kisuni na kuondoa uanachama wake katika chama cha National Islam. Wauaji wote watatu walikuwa wanachama wa chama cha National Islam.
8. ROBERT F. KENNEDY
Mdogo wa raisi aliyeuwawa wa marekani John kennedy. Aliuawa mwaka 1968 miaka mitano tu baada ya kaka yake kuuliwa. Ilikuwa pia ni miaka mitatu toka kuuliwa kwa mwanaharakati Malcom X na miezi kadhaa baada ya kuuliwa kwa Mwanaharakati mwingine Martin Luther king Jr. Ulikuwa ni mfululizo wa mauaji ikumbukwe kuwa hata Patrice Lumumba wa DRC nae aliuawa mwaka 1961 (miaka 7 kabla).
9. TUPAC OMAR SHAKUR
Hili si jina geni kwa mtu yeyote mpenzi wa muziki hasa miondoko ya hiphop. Aliyepigwa Septemba 7, 1996 akitoka Las vegas Navada alikokwenda kuhudhuria pambano la Mike Tyson. Akiwa na Meneja wake Suge Knight (ambae pia anahusishwa na kifo hicho).
2pac aliuwa kwa kupigwa risasi kadhaa kifuani zilizotoka kwenye gari moja nyeupe iliyowazuia kwa pembeni.
2pac alifariki siku chache baadae katika hospitali ya University Medical Center of Southern Nevada.
Wengi walihusishwa na kifo chake huku idadi kubwa ikimuelekea Christopher wales (B.I.G) kuwa ndiye aliehusika moja kwa moja na kifo caha 2pac. B.I.G aliuawa miezi sita baadae na watu waliodaiwa kuwa ni mashabiki wa 2pac kwa lengo la kulipa kisasi
10. JUVÉNAL HABYARIMANA
Aliuawa baada ya ndege yake kushambuliwa na kuua watu wote waliokuwemo kwenye ndege hiyo akiwemo raisi wa wakati huo wa Burundi. Mauaji hayo ndiyo yalioamsha hasira za wanyarwanda hasa wahutu na kuanzisha vita dhidi ya watutsi na baadae mauaji ya kimbari.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na ufaransa, mauaji hayo yamefanywa na chama cha Rwandan Patriotic Front (RPC) na kumuhusisha raisi wa sasa wa rwanda paul Kagame ingawa kagame mwenyewe amekuwa akikemea vikali na kusema wafaransa wanajaribu tu kuficha uovu wao!