Diamond asema – Ni kweli Mzee Abdul sio Baba yangu
“Ni kweli Mzee Abdul si baba yangu mzazi, Lakini tangu mtoto nilikua nampenda sana . Mpaka Mwaka 2000 ndio Mama yake RJ The DJ akaniambia ukweli ..
Hakuna mtu ambae alikua anajua ukweli kwasababu Ndugu zangu wote niliwakusanya kwa Upendo, Kuanzia wakina Ricardo na Queen Darlin”
RELATED: Baba Levo Ft Diamond Platnumz – Shusha
“Hata baada ya Kujua Ukweli bado Mapenzi yangu makubwa yalibaki kwa Mzee Abdul kama baba yangu ..
Kwa bahati mbaya yeye aliniweka mbali sana, na nadhani kuna Kipindi mama yangu alichukia kitendo cha yeye kusema kwenye vyombo vya Habari kuwa simsaidii Lakini Kiukweli nimekua namsaidia ” – Diamond Platnumz
Source: Wasafi Fm