Kama tunavyojua ndugu zetu na majarani zetu Watanzania walikuwa katika harakati za uchaguzi mkuu na siku chache zilizopita walipiga kura kuchagua wabunge, wadiwani na Rais na hayo ndio matokeo.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemtangaza aliyekuwa mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM Dkt .John Pombe Magufuli kuwa mshindi wa nafasi hiyo baada ya kupata kura 12,516,252 akifuatiwa na Tundu Lissu wa CHADEMA mwenye kura 1,933,271.
Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) imemtangaza mgombea wa urais wa Zanzibar kupitia CCM, Dk Hussein Mwinyi kuwa mshindi wa kiti hicho kwa kupata kura 380,402 sawa na asilimia 76.27 ya kura zote.
Akitangaza matokeo hayo mwenyekiti wa ZEC, Jaji Hamid Mahamoud Hamid amesema wagombea urais walikuwa 17 waliopigiwa kura 498,786 sawa na asilimia 88.07 ya wapiga kura 566,352 waliojiandikisha.