MAKALA

Siku za kupata au kushika mimba (Jifunze hapa)

Siku za kupata au kushika mimba (Jifunze hapa)

Mara nyingi wanawake huamini kuwa yai huachiliwa katikati ya mzunguko wa hedhi. Ukweli ni kwamba yai huachiliwa siku 12 hadi 16 kabla ya mzunguko unaofuata kuanza.

Ijapokuwa kwa mwanamke mwenye mzunguko wa siku 28 yai lake laweza kuachiliwa katikati ya hedhiย (kati ya siku ya 12 na 16),ย mwanamke mwenye mzunguko wa hedhi wenye siku 36 yai lake huachiliwaย kati ya siku 20 na 24.

RELATED: Dalili za kwanza za mimba changa โ€“ wiki moja na kuendelea.

Kwa wanawake wenye mizinguko isiyobadilika sana, njia nzuri ya kukadiria siku ya yai kuachiliwa niย kutoa 16ย kutoka kwenye jumla ya siku za mzunguko wake wote na baada ya kupata jibu, ajumlishe jawabu hilo na 4.

Hii itampa siku ambayo yai huweza kuachiliwa.

Kwa mfano, mwanamke mwenye mzunguko wenyeย siku 22ย mara nyingi yai lake huachiliwa kati yaย siku ya 6 hadi 10 ya mzunguko wake (22-16=6, halafu 6+4=10).

Onana na Daktari wako kwa msaada zaidi.

Siku za kupata au kushika mimba (Jifunze hapa)

Leave a Comment