Wiki chache zilizopita mkali wa muziki wa rap kutoka toronto, Drake alikichafua kwenye mitando baada ya kuonesha sehemu ya mjengo wake mpya alioujenga nyumbani kwao Toronto Canada.
Mjengo huo wa Drake ambao umetengenezwa na mbunifu wa majengo Ferris Rafauli una futi za mraba 50,000 ukiwa na vitu vya kifahari vingi kama uwanja wa mpira wa kikapu ndani wenye ukubwa sawa na viwanja vya nba, studio kubwa ya muziki.
Drake mwenyewe ameifananisha studio hiyo na studio za miaka ya 1970 iliyochangwanya na muundo wa club ya Annabel ya London, moja ya club za kifahari zaidi duniani.
Chumba cha tuzo ambacho kimejumuisha mafanikio yake tangu utotoni, alivyokuwa anaigiza kwenye Tv show ya “Degrassi: The next generation” hadi tuzo za grammy, ukumbi wa jerseys za michezo, gym, chumba cha piano, garage ya magari 10 ndani na dimbwi la kuogelea la ndani.
Chumba cha drake kimepambwa na kitanda chenye thamani ya dola 395 zaidi ya Tsh. Millioni 900 za kitanzania, sasa now you know why kwenye wimbo wa god’s plan aliimba “I only love my bed and my momma I’m sorry”.
“Kwa sababu nilikuwa naijenga kwenye mji wangu, nilitaka muundo ambao utasimama kwa miaka 100. Nilitaka huwe mjengo mkubwa, utakuwa moja ya mambo ambayo nitaayaacha, kwa hivyo ilikuwa ni lazima huwe imara na wa muda wote” Drake amewahi kuelezea
Jengo hilo la kifahari ambalo amelipa jina la “The embassy” yaani ubalozi limejengwa kwa viwango na muundo vya majengo ya miaka ya karne ya 19 lakini muundo wa ndani umetengenezwa kisasa.
Mjengo huo unaripotiwa kuzungukwa na kuta ndefu yenye urefu wa mita 4.4 ambapo drake alilazimika kuomba idhini serikalini kwasababu sheria za jiji hilo haziruhusu kuta za makazi zinazozidi mita mbili kwa urefu.
Drake ameuonesha mjengo wake kwenye video ya “Money in the grave”, akauonesha tena kwenye video ya “Chicago freestyle/ when to say when” na pia video ya wimbo wa “Toosie slide”
Tazama video hapo chini kwa habari kamili…