ENTERTAINMENT

WCB Wasafi wamsaini msanii mpya mwanadada Zuchu

Mnamo tarehe 7/04/20 Diamond Platnmuz alitoa-tamko kwamba siku ya leo WCB wasafi watamtangaza msanii mpya ambaye atajiunga katika kundi la hilo.

Hayawi hayawi sasa yamekuwa, kiongozi wa kundi wa WCB Diamond Platnumz amemtangaza msanii mpya siku ya leo, ambaye amejiunga rasmi na kuwa mwanafamilia wa WCB wasifi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Diamond Platnmuz amemtangaza mwanadada ZUCHU kama mwanafamilia mpya wa WCB wasafi.

Sababu ziliwapolekea wao kumsaini mwanadada huyu ni uwezo mkubwa wa utunzi alionao, pia na sauti iliyotulia.

Diamond Platnmuz amesema ZUCHU ni zaidi ya kipaji, huku Direct Kenny naye ametia neno na kusema ZUCHU anamwonekano mzuri sana.

Leave a Comment