Moja kati ya stori zilizochukua headlines siku ya jana 08/04/2020 ni stori ya WCB kumsaini rasmi mwanadada Zuchu, ambaye ni mtoto wa Khadija Kopaa.
Familia ya WCB Wasafi wakiongozwa na CEO wao Diamond Platnmuz walimtambulisha rasmi Zuchu kama msanii mpya katika kundi hilo.
Baada ya kutambulishwa hii ndio kauli ya kwanza ya mwanadada Zuchu, huku akitoa shukrani za dhati kwa Diamond Platnmuz.
“It’s a huge Honor to finally fulfill My Dream, Na pia ni baraka na bahati kubwa sana to be signed under The Biggest Label In Africa @wcb_wasafi
Nikiwa kama mwanamke ndoto yangu kubwa ni kutumia kipaji changu kuthibitisha ule usemi “Power’s not given to you. You have to take it” yaani “Nguvu Haiji Kwa Kupewa, Bali Kwa Kujitengenezea Mwenyewe”.
Na hii ni ili kufuta imani na dhana potofu kuwa wanawake hawawezi bila ya kuwezeshwa.
Na muhimu zaidi pia safari yangu katika muziki iende kuwatia nguvu wanawake wote kupambana katika kutimiza ndoto zao.
Kwa zaidi ya miaka minne niliisubiri siku hii.
Thank you @diamondplatnumz and whole of @wcb_wasafi Management for believing in my talent. Expect The Absolute Best.
To All Music Lovers from All Over The World, Ninaitegemea sana support yenu.
Asante Mwenyezi Mungu kwa kipaji na nafasi hii, Ninakuomba uniongoze katika njia yenye Mafanikio. Zuchu #WCB4LIFE” – Alisema Zuchu kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Maneno ya kwanza ya Zuchu baada ya kutangazwa WCB rasmi