ENTERTAINMENT

Dawa ya kubana UKE uwe MNATO wenye kuleta msisimko zaidi

kubana UKE uwe MNATO wenye kuleta msisimko zaidi

Kama wewe ni msichana au mwanamke ambaye hujawahi kuzaa hata mara moja, suala la wewe kuwa na uchi mpana ni la kufikirika, uwezekano ni mdogo mno au ni finyu.

Kuna dhana iliyoenea kwamba mwanamke anayeshiriki ngono sana atakuwa na uchi uliolegea – Huu ni Upuuzi kabisa!

Mwanamke hata akifanya ngono kiasi gani, uchi hauwezi kuwa mpana eti kwa sababu hiyo. Sababu kubwa ya kuwa na uchi uliolegea kwa mwanamke ni tendo la Uzazi.

Mwanamke anapozaa misuli inayozunguka uchi na vitu vyote vinavyoshikilia kuta za uchi huo huathirika na kupungua nguvu kwa kiasi fulani.

Hivyo basi, kila unapozaa, ndivyo unavyoiathiri misuli yako zaidi.

Mwanamke mwenye watoto wengi sana, uchi wake utakuwa umeathirika zaidi. Namna ulivyozaa pia inaweza kuchangia, kwa mfano kuzaa kwa matatizo (Plonged labours).

Tiba ya tatizo La Uchi Kulegea Njia iliyo bora kabisa ni kuwa makini kwa kufanya mazoezi unayopewa au kufundishwa na wakunga (manesi) mara tu baada ya kuzaa.

Lakini endapo mambo yameshaharibika, basi yafuatayo yaweza kufanyika.

1. Kufanya mazoezi yaitwayo Pelvic Floor Muscle Exercises .
Haya ni mazoezi ambayo manesi au wakunga wanaweza pia kukufundisha.

2. Kufanya mazoezi ya Kegel.
Mazoezi haya huipa nguvu misuli (Pelvic Floor Muscles) iliyovutika wakati wa uzazi.

Hukufanya usikie raha zaidi ufanyapo tendo la ndoa (more intense orgasms) na huimarisha mfuko wa mkojo ili usivuje.

Mazoezi haya hayapunguzi ukubwa wa uchi bali hupunguza kipenyo cha uchi sehemu ya kuingilia.

3. Njia nyingine ni kutumia vaginal muscle developers, vaginal cones, neuromuscular electrical stimulation na neocontrol.

Hivi ni kwa wale ambao watakuwa na uwezo wa kuagiza vifaa hivi kutoka nje.

Wanawake wa mataifa mbalimbali ulimwenguni wamekuwa wakitumia njia mbalimbali kupambana na tatizo hili.

Wanawake wa visiwa vya Madura huko Indonesia kwa karne nyingi wamekuwa wakitumia dawa iliyotengenezwa kutokana na majani yanayopatikana katika msitu ya visiwa hivyo.

Leave a Comment