Ni jana tu tulikutaarifa kuhusu Diamond Platnumz kutangaza kuwa atatoa msaada wa kulipia kodi ya pango kwa Familia 500 katika kipindi hiki kigumu.
Huwenda swala hilo limemfiki mzazi mwenza wa Diamond Platnumz kwa watoto wawili, Zari The Boss Lady ambaye kwa mara kadhaa amekuwa akimtuhumu diamond kwa kutokutoa matumizi kwa watoto wake wanaishi South Africa.
Zari ametumia ukurasa wake wa instagram kuandika ujumbe mrefu na mzito ”…. But you dont know what your kids eat, or how they sleep, if fees and medical insurance is paid.
You will never please the world when your own are not happy & taken care of. Your selling a lie.
Isikupite hii: Diamond Platnumz kulipia familia 500 kodi za nyumba miezi 3
Some people have become clowns to some of us…. ” – Zari The Boss Lady
Ujumbe huu kwa wengi umechukuliwa kuwa kama ujumbe wake kwa diamond kuwa amekuwa sio mtu wakutoa matumizi kwa watoto wake na hajui hata wanalalaje, wanakulaa nini tafsiri ya ujumbe huyo.
Lakini hujui watoto wako wanakula nini, au wanalala vipi, ikiwa ada na bima ya matibabu hulipwa. Kamwe hautawahi kufurahisha ulimwengu wakati wako hawafurahi na kutunzwa. Unajidanganya.
Watu wengine wamekuwa Clowns kwa wengine wetu….” Kauli yako kama nishabiki ni ipi katika hili