Wema Sepetu amesema anaanza kutoa darasa la mapishi kwa kupitia App yake ya @wemaapp.
Amefunguka na kusema jinsi ambavyo watu wengi wamekuwa wakisifia chakula anachopika, ameona ni bora sasa akatumia nafasi hiyo kuingiza kipato.
โHivyo nimeona bora niitumie hii nafasi kuanzisha darasa la mapishi ambalo litakuwa likiruka kwenye app yangu ya @wemaapp kila wiki, kwa hiyo wale mashabiki wangu wa dhati wakae mkao wa kula,โ alisema Wema.