Uncategorized

Maswali manne mazuri ya kumuuliza mwanamke

Maswali manne mazuri ya kumuuliza mwanamke

1. Kawaida unafanya nini siku za wikendi?
Hili ni swali lililowazi ambalo unaweza kumuuliza mwanamke yeyote ili kuzua mjadala zaidi. Iwapo ashaeleza katika profile  yake, basi unaweza kulijeuza swali hilo na kumuuliza zaidi kuhusu mambo anayoyafanya wikendi. Mfano kama ameeleza kuwa wikendi yeye hupenda kupika unamuuliza ni chakula gani na kadhalika. Hivi utamfanya akuelezi mengi na mengi huku ukimakinika kwa kuchukua yote ambayo atakutajia ili baadae utumie hio nafasi kuuliza maswali zaidi. Pia unaweza kutumia hii nafasi uangalie vitu ambavyo vinafanana na mnavipenda nyote wawili.

2. Ushawahi kukutana na mwanamume yeyote kwa mtandao ambaye humpendi?
Hili ni swali muhimu la kumuuliza mwanamke kwani litakusaidia wewe kujitenga na kujitofautisha na wanaume wengine wanaopatikana kwa mtandao wa kijamii. Kumuuliza swali hili litamfanya kufungua roho yake kwako kwani ataona ya kwamba wewe unaelewa tofauti na changamoto ambazo zinapatikana kwa wanawake kutoka kwa wanaume. Hii kwa muda mfupi utamwona mwanamke kama huyu akiingiwa na ari ya kutaka kukujua zaidi na zaidi.

3. Je wapenda date zinazofanyika online?
Hapa lazima utumie ujanja wakati wakuuliza swali kama hili. Jaribu kutumia mbinu ya kujeuza jeuza na kuchezea maneno ilimradi uzue maswala mengi ambayo yatazunguka katika hili swali. Mfano baada ya kumuuliza unaweza kuuliza maswali kama nani, wapi, ilikuwaje, halafu nk ili kufanya maongezi yenyewe yawe na mnato wake.

Jaribu kumakinika kadri uwezavyo na unukuu mambo ambayo tayari amepitia ili kujaribu kufananisha na yako.

4. Vitu gani unavyopenda na kuchukia?
Fanya kumuuliza hili swali ili upate kuyajua mambo yake . Hii itakuwasaidia wewe kuweka mipaka kwa mambo ambayo yanaweza kumkwaza ama kumfurahisha.

KUMBUKA: Kulingana na utafiti ni kuwa ndoa nyingi ambazo zinatokana na mitandao ya kijamii hufanikiwa zaidi kuliko ndoa nyingine zozote zile.
Pia fahamu ya kwamba maswali manne hapo juu yanaweza kubadilishwa ili yatumike kulingana na changamoto unazoziona wewe.

Leave a Comment