1. Kwa mpenzi wangu, wewe ni mwanamke mrembo zaidi kuliko kiumbe chochote katika maisha yangu. Nakupenda zaidi ya kitu chochote ama yeyote. Ndoto yangu ni kuwa penzi letu litaendelea kuwa na nguvu kadri siku zinavyosongea.
2. Wewe ni mpenzi wangu na umenipatia sababu milioni kwa mimi kutabasamu kila siku.
3. Kwa sababu ya penzi lako, mpenzi wangu, naweza kuukwea mlima mrefu zaidi na pia kutatua matatizo makubwa zaidi. Penzi lako kwangu linayapa maisha yangu sababu za kufanikiwa.
4. Nikiwa na wewe ubavuni mwangu na penzi lako likizunguka moyo wangu, naweza kufanikiwa na chochote. Unanipa nguvu na nishati ya kukabiliana na chochote. Nakupenda kwa moyo na roho yangu.
5. Bila penzi lako katika maisha yangu, maisha yanakuwa ya upweke na kiza. Wewe ndie unayeleta mwangaza na rangi ya upinde kwa maisha yangu, hata kama ni nyakati za mawingu. Asante sana mpenzi wangu.
6. Furaha inapulizwa katika maisha yangu wakati unaponitabasamia. Unapoongea, sauti yako ina nguvu ya kunipeleka sehemu ambayo kuna upendo na amani.
7. Wewe ni mpenzi wangu bora zaidi. Wewe ni zawadi ambayo nimeletewa na Mwenyezi Mungu na nitaitunza na kuilinda daima.
8. Mapenzi yako huyafanya maisha yangu kuwa ya mwangaza na kuvutia. Hujaacha kuamini uwezo wangu wa kutimiza mambo na kwa sababu ya hilo nakuthamini.
9. Kila dakika ninayochukua nikiwa na wewe huwa ni spesho. Tunagawa hisia zetu na maisha yetu pamoja. Hivyo napenda zile hisia zote ambazo tunakuwa nazo wakati huo. Nakupenda mpenzi wangu.
10. Nikikuweka mikononi mwangu, nahisi amani ikizunguka katika kumbata letu. Nakupenda na utakuwa karibu yangu kila wakati.
11. Kila kitu kimekamilika katika dunia yangu, hii ni kwa sababu ya penzi letu ambalo tunagawa.
12. Kila nikifunga macho yangu huwa nakuona mbele yangu. Kutengana kimwili hakuwezi kuzuia penzi letu ambalo tunalithamini tangu jadi.
13. Haijalishi mahali popote ulipo kwa kuwa mara kwa mara unakuwa ndani ya moyo wangu na fikra zangu.
14. Siku yangu huanza kwa kukufikiria wewe mpenzi wangu na huishia hivyo hivyo. Nakupenda wangu laazizi.
15. Kama ningepewa nichague kati ya kulia na wewe ama kutabasamu na mwingine, ningekuchagua wewe kila wakati. Wewe ni penzi la maisha yangu.
16. Wewe ni zaidi ya mwanamke bora kwangu, wewe ni kila kitu kwangu. Nakupenda kwa moyo wangu wote.
17. Maneno hayaji kirahisi, lakini ninapokuwa na wewe, moyo wangu unadunda kwa haraka na nyota zinangaa zaidi.
18. Laazizi wangu, wewe ni zaidi ya mchumba wangu, kila siku ni wewe unayeleta furaha ndani yangu siku baada ya siku.
19. Wewe ni chuma katika ngao yangu, upepo katika dau langu na mdundo katika moyo wangu.
20. Kwa mahabuba wangu, mpenzi wangu ninayempenda, tumekamilika tukiwa pamoja. Asante kwa kugawa maisha yako na mimi.
21. Natamani niwe kitu cha kwanza ambacho unafikiria pindi unapoamka, mpenzi wangu.
22. Itakuwa fahari yangu iwapo nitakuwa mtu wa mwisho kumfirikia kabla hujaenda kulala.
23. Una uwezo wa kumwilika maisha yangu kama vile unavyonifanyia kila siku. Nakupenda.
24. Unafanya dunia yangu kuzunguka na kuzunguka kila siku. Sijui nitafanya nini bila wewe.
25. Mpenzi wangu nakuhitaji kama vile moyo wangu unavyohitaji kudunda.
26. Siamini wanaposema kuwa kuna kitu kinachoitwa kupenda kwa kuona mara ya kwanza kwa sababu kila nikikuona nakupenda zaidi na zaidi.
27. Kama mimi ni mfalme katika himaya yangu, basi himaya yangu haiwezi kukamilika kama wewe hautakuwa kando yangu kama malkia.
28. Kama ningepewa nguvu za kuweza kurudisha kumbukumbu za awali, basi ningerudisha hadi ile siku ya kwanza nilipokuangalia machoni na nikakuangukia kwa kukupenda. Nakupenda mpenzi wangu.
29. Hata kama nimeshindwa kuwa chozi lako, na pia kushindwa kuwa tabasamu lako, lakini kwako umefaulu kuwa hewa yangu ambayo inanifanya kuwa hai kila siku.
30. Nataka kuwa hewa ambayo inakuzunguka kila mahali. Nataka nisitambulike lakini niwe na umuhimu zaidi kwako. Nakupenda.
sanaz maize bila anady