ENTERTAINMENT

Wafahamu wanasayansi waliogundua virusi vya UKIMWI

Wafahamu wanasayansi waliogundua virusi vya UKIMWI

Wafahamu wanasayansi waliogundua virusi vya UKIMWI Luc Montagnier na Robert Gall.

Jinsi alivyogundua virusi vya ukimwi

Mwaka 1982, Willy Rozenbaum, daktari katika hospitali ya Hôpital Bichat mjini Paris, alimuomba msaada Montagnier kugundua kitu kinachosababisha ugonjwa mpya ambao haukujulikana kwa wakati ule, ambao leo ndiyo UKIMWI.

Kwa wakati ule waliuita (Gay Related Immune Deficiency), ambapo kwa wakati mwingine Mwanasayansi Rozenbaum alipendekeza katika mkutano wa wanasayansi kwamba sababu ya ugonjwa inaweza kuwa retrovirus (aina ya virusi).

Montagnier na timu yake walikuwa na uzoefu wa kina na virusi aina ya Retroviruse. Montagnier na timu yake walichunguza sampuli zilizochukuliwa kutoka kwa wagonjwa wa UKIMWI wa Rozenbaum na kupatikana virusi ambavyo baadae vilijulikana kama “lymphadenopathy-associated virus” (LAV), kwani ilikuwa bado haijajulikana kuwa ndivyo vilikua chanzo cha UKIMWI, na baadae walichapisha matokeo yao katika jarida la Sayansi mwaka 1983.

LUC MONTAGNIER

Luc Montagnier Antoine alizaliwa 18 Agosti 1932, ni mfaransa na mtaalamu wa Sayansi ya virusi na alipewa tuzo ya heshima ya Nobel ya tiba ya mwaka 2008 pamoja na Françoise Barré-Sinoussi na Harald zur Hausen kutokana na ugunduzi wake wa virusi vinavyosababisha Upungufu wa Kinga mwilini yaani Virus vya Ukimwi  (VVU).

Kwa muda mrefu alikuwa mtafiti katika Taasisi ya Pasteur katika jiji la Paris Nchini Ufaransa, yeye kwa sasa anafanya kazi kama profesa wa muda katika Chuo kikuu cha Shanghai Jiao Tong nchini China.

ROBERT GALLO

Baadae timu iliyoongozwa na Robert Gallo aliyezaliwa  March 23, 1937, Mwanasayansi kutoka Marekani ilichapisha matokeo sawa na ya Montagnier katika suala hilo hilo la Sayansi ya virusi, na baadaye alithibitisha ugunduzi wa virusi na kuwasilisha ushahidi kwamba virusi hivyo vinasababishwa UKIMWI.

Leave a Comment