Msanii wa Bongo Fleva Lina Sanga amefunguka na kusema hasikii wivu wala haimuumizi kuona rafiki yake Nandy ameolewa na aliyekuwa mpenzi wake Billnas.
Linah amefunguka hayo akiwa mjini Songea akiwa ni mmoja wa wasanii walioshiriki kwenye tamasha la Nandy Festival,ambapo cuople hiyo ndo wahusika wakuu.
“Kwani mtu akiwa ex wako inatakiwa awe ni adui?hata kama tulikuwa pamoja ni muda mrefu umepita na ndo mana huwa sipendi kuliongelea sana.Huu si muda wa kujadili mambo ambayo yalishapita na haya make sense ,Nandy ni mdogo wangu na Nenga ni mshikaji wangu ,niko na amani” Alifunguka Lini
Linah na Billnas waliwahi kuwa wapenzi hapo zamani kabla ya rapa huyo kuhamia kwa mwanadada Nandy.