Kumekuwepo na tetesi nyingi sana za chini chini kuwepo kwa bifu kati ya wasanii wawili wa kike wakubwa hapa nchini ,Nandy na Zuchu.
Hata hivyo kila mmoja alipohojiwa kwenye media alikana kuwa na tatizo na mwenzake.Tetesi hizo za bifu kati ya wawili hao zimechukua sura mpya siku za hivi karibuni baada ya kuvuja kwa sauti ya mwanadada anayesadikiwa kuwa ni Nandy akitengeneza fitna Dhidi ya Zuchu.
RELATED : Esma Platnumz Afunguka Kuhusu Sauti yake ya Mahaba Iliyovuja.
Katika Sauti hiyo iliyorekodiwa na kuvuja inasikika sauti ya anayedaiwa kuwa ni Nandy akiongea na mwijaku kuwa afanye manuva kwenye story ya dili fulani la ubalozi ambalo Zuchu anadai kuwa alikataa kwa sababu hakutaka kutangaza pombe na kusemekana kuwa baaada ya Zuchu kukataa ndio dili hilo likamwangukia bi dada Nandy.
Katika clip hiyo ya sauti Inaonekana kuwa Nandy anamwelekeza Mwijaku aiboreshe hiyo story isionekane kuwa yeye alipewe dili baada ya Zuchu kuikataa ,bali ionekane kwamba aliipambania na aliipata kutokana na kuwa yeye ni msanii mkubwa kuliko zuchu.
Katika sauti hyo anayesadikiwa kuwa ni Nandy alisikika akisema “Yani Mtu akatae dili la hela nyingi kwa sababu eti ni pombe?
Inasadikika kuwa Nandy aliumizwa na kitendo cha Zuchu kusema kuwa alikataa kufanya kazi na kampuni ya pombe na baada ya yeye kukataa ndio Nandy akapewa dili hilo kitu kinachoashiria kuwa pengine Zuchu ni msanii mkubwa kuliko Nandy.
Wakati hayo yakiendelea ikatokea sauti nyingine ambayo anasikika akiongea mtu ambaye watu wanadai kuwa ni Mwijaku akisema kuwa Nandy alikuwa anataka kumlipa pesa takribani milioni 1.8 ili tu afanye manuva ya story hiyo na kuivujisha mtandaoni kitu ambacho yeye alikataa.
“Alitaka kunilipa Tsh milioni 1.8 ili nipost kwenye ukarasa wangu ,me nikamwambia hapana,kama utanipa pesa kama kaka yako sio kumzungumzia mtu.Zuchu ni kijana mdogo na anapambana …” alisikika Mwijaku.
Hata hivyo inasemekana kuwa kumekuwa hakuna maelewano mazuri kati ya Nandy na Mwijaku kitu kilichofanya Mwijaku avujishe sauti hiyo.
Also, check more tracks from Nandy;