Rayvanny – Kwetu LYRICS
Sifa kwa Mola wangu Maulana
Kwa mengi aliofanya
Hadi mi na we kukutana, kisura
Sijapanga kudanganya
Nasema ukweli mama
Kisa nakupenda sana, kisura
Umesema wanipenda
Ila maisha yangu maseke
Michicha milenda
Menu yangu na ya kuku mateke
Yaani chenga
Kila siku kilio saa lini nicheke
Sina tenda
Ugali Buguruni mboga Temeke
Nafurahi umeniridhia
Niwe na wewe kimwali
Maisha yangu mitihani
Isoisha maswali
Ukifika nyumbani vumilia
Maana hali sio swali
Asubuhi mchana pakavu
Jioni ndo kula futali
Tena
Huku kwetu
Muda wowote mateja wanatinga
Viwalo vyetu
Ukifua kumbuka kuvilinda
Huku kwetu
Muda wowote mateja wanatinga
Mwali wee
Suala la nyumba na gari mi
Bado, mi bado, mi bado
Ndo kwanza nimepanga
Bado, iyee, mi bado
Sina hata kiwanja
Bado, iyee, mi bado
Kulipa kodi majanga
Bado, mimi bado, mi bado
Mtaani kwetu hekaheka ukienda sokoni kariri vichochoro
Ghetto namkeka tu hakuna kitanda, shuka wala godoro
Hekaheka hakuna kibatari ndani giza totoro
Mvua ikinyesha nyumba inageuka ka boti ya Comoro
Ila nimeshakupa
Nimeshakupa mtima mtima
Ukija kususa
Utanizika mzima mzima
Nimeshakupa eh
Nimeshakupa mtima mtima
Ukija kususa
Utanizika mzima mzima
Tena
Huku kwetu
Muda wowote mateja wanatinga
Viwalo vyetu
Ukifua kumbuka kuvilinda
Huku kwetu
Muda wowote mateja wanatinga
Mwali wee
Suala la nyumba na gari mi
Bado, mi bado, mi bado
Ndo kwanza nimepanga
Bado, iyee, mi bado
Sina hata kiwanja
Bado, mie, mi bado
Kulipa kodi majanga
Bado, mimi bado, mi bado
Also, check more tracks from Rayvanny;