Mbosso atangaza kuchia kolabo 5 za Kimataifa
Staa wa muziki wa bongo Fleva na msanii kutoka katika lebo ya WCB Wasafi, Mbosso ametangaza kuwa tayari amekamilisha kolabo tano na wasanii wa kimataifa.
RELATED: Mbosso Ft Diamond Platnumz – Karibu (Prod. Abbah)
Msanii huyo aliweka taarifa hiyo wazi kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa kwa siku za hivi karibuni alikuwa mjini Lagos, Naijeria ambako pia alikuwa akifanya kazi ya kimuziki.
Mbosso alitoa shukrani za dhati kwa wadau tofauti wa muziki kutoka Lagos kwa mapokezi mazuri waliyompa. Baada ya ujumbe huo, Mbosso, vile vile, alichapisha picha za bendera ya taifa la Komoros, kuashiria kuwa huenda ameelekea huko au anafanya kazi ya kimuziki na wadau kutoka taifa hilo.
“Lagos has been real. The vibes and energy was crazy. I have 5 global hits. Hits collabos coming your way. Keep it locked here,” ujumbe wa Mbosso mtandaoni ulisomeka.
Hata hivyo supa-staa huyu hakutaja majina ya wasanii aliofanya kolabo nao au mataifa wanakotoka. Ikumbukwe kuwa mwaka jana, tuhuma ziliibuka mtandaoni kuhusu ujio wa kolabo baina ya Mbosso na msanii wa Kenya Mr. Seed.
Hii ilikua baada ya picha zilizowaonyesha wawili hao wakiwa studioni kuvuja mtandaoni. Kwa sasa, mashabiki wa Mbosso wamebaki na hamu kuhusu ujio wa kolabo hizo.
Kwa mwaka huu, Mbosso ameacha kazi moja tu ambayo ni ‘Tausi’, aliyomshirikisha Mrisho Mpoto.
RELATED: Macvoice Ft Mbosso – Only You (Prod. Mocco)
Kabla ya hapo, mwishoni mwaka jana aliachia ‘For You’ aliyomshirikisha Zuchu. Kazi zote zilipata mapokezi mazuri.
Also, check more tracks from Mbosso;